Tottenham wanataka kumsajili beki wa Real Madrid na Ujerumani Antonio Rudiger, 29, katika dirisha la usajili la kiangazi. (Fijaches)
Manchester United wako tayari kuongeza mshahara wa David de Gea hadi kufikia £250,000 kwa wiki ili kumbakisha kipa huyo wa Uhispania mwenye umri wa miaka 32 Old Trafford, lakini klabu hiyo tayari inamtazama mlinda mlango wa Leeds Mfaransa Illan Meslier, 22, kama mbadala wake wa muda mrefu. (Sun)
Ofa ya Sir Jim Ratcliffe ya Manchester United ya kuinunua Manchester United ni £1bn chini ya £5bn iliyotolewa na Sheikh Jassim Bin Hamad Al Thani. (Foot Mercato)
West Ham wanaweza kutuma ofa za kumnunua kiungo wa kati wa Manchester United na Scotland mwenye umri wa miaka 26 Scott McTominay, beki wa kati wa England Harry Maguire, 29, kiungo wa kati wa Uholanzi Donny van de Beek, 25, na mshambuliaji wa Ufaransa Anthony Martial, 27. (CaughtOffside).
The Hammers wamemuweka kiungo wa kati wa Lazio na Serbia Sergej Milinkovic-Savic, 27, kwenye orodha yao ya kipaumbele kuchukua nafasi ya kiungo wa kati wa England Declan Rice, iwapo mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 ataondoka msimu wa joto. (Sun)
Manchester City wanapanga kufanya mazungumzo na mshindi wa Kombe la Dunia wa Argentina, Julian Alvarez kuhusu kandarasi mpya, licha ya mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 23 kuwasili Etihad msimu uliopita wa joto. (Mirror)
Wawekezaji wa Qatar wanaweza kutoa ofa ya kunua hisa Tottenham, hata kama Sheikh Jassim Bin Hamad Al Thani atakamilisha kuinunua Manchester United. (Times)
Newcastle United wanapanga kumnunua beki wa pembeni wa Fulham na Marekani Antonee Robinson, 25. (Football Insider)
Barcelona ilikubali kumsajili mshambuliaji wa Atletico Madrid na Ureno Joao Felix Januari 2022, lakini dili hilo lilikwama kwa sababu ya kanuni za fedha za Financial Fair Play (FFP). (AS)
Kiungo wa kati wa Nottingham Forest Muingereza Lewis O'Brien, 24, anazivutia klabu za ligi ya Marekani (MLS) za New York City, Columbus Crew na Atlanta United. (Sun)
Liverpool wameanza mazungumzo ya awali juu ya kumsajili beki wa Colombia chini ya miaka 20 Kevin Mantilla, 19, kutoka Independiente Santa Fe. (Football Insider)
Crystal Palace na West Ham wanatamani kumnunua kiungo wa kati wa Bristol City na Uingereza Alex Scott, 19, ambaye thamani yake ni pauni milioni 20. (Sun)
BBC