Rais wa Yanga Injinia Hersi Said amesema mchezaji Bernard Morrison alipata majeraha wakati akiitumikia klabu hiyo hivyo ni wajibu wao kumuhudumia
Hersi amesema inawezekana Yanga bado haijanufaika na mchezaji huyo ambaye analipwa fedha nyingi lakini hawawezi kukwepa wajibu wao
"Bernard Morrison analipwa fedha nyingi, uzoefu wake ni mkubwa kwenye mashindano ya Kimataifa anaweza kuwa mchango mkubwa sana"
"Yanga imemrudisha kwenye msimu huu ile 'impact' ambayo watu walikuwa wakiitegemea haijatokea hapo sasa ndio suala la mkataba linapokuja"
"Mchezaji ana mkataba na unatakiwa kuuheshimu. Atalipwa awe anacheza au hachezi. Mchezaji ameumia lakini wakati anasajiliwa alikuwa mzima"
"Ameumia wakati akiitumikia Yanga. Mchezaji akiumia hawezi kucheza. Hiyo haiepukiki, Morrison sisi kama Yanga tunamuhudumia na huu ndio uungwana ambao Yanga tunao"
"Na tunamuhudumia kuhakikisha anakuwa bora kuelekea mwisho wa msimu au kwenye future ya kipaji chake. Alipata majeraha na tulimpeleka Tunisia," alisema Hersi