Kesho Jumatano Februari 22 KMC itakuwa mwenyeji wa Yanga katika mchezo wa ligi kuu utakaopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa
KMC wametangaza viingilio vya mchezo huo utakaopigwa saa 10 jioni. VIP A ni Tsh 15,000/-, VIP B ni Tsh 10,000/- na Mzunguuko ni Tsh 5,000/-
Ni mechi muhimu kwa kila timu KMC wakihitaji ushindi ili kujiondoa kwenye hatari ya kushuka daraja wakati Yanga inataka kushinda ili kuendeleza ubabe wake kwenye ligi wakiwa pia wanawania kutetea ubingwa wao kwa msimu wa pili mfululizo
Ni wazi, hautakuwa mchezo mwepesi kwa KMC kwani wanakutana na Yanga ambayo imetoka kuigaraza TP Mazembe mabao 3-1 katika mchezo wa kombe la Shirikisho barani Afrika



