Mtanange wa ligi kuu kati ya Simba dhidi ya Azam Fc uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa, umemalizika kwa matokeo ya sare ya bao 1-1
Bao la sekunde ya 14 lililofungwa na Prince Dube liliiweka Azam Fc katika nafasi nzuri katika mchezo ambao licha ya Simba kutawala ilikuwa sio rahisi kwao kuweka mpira nyavuni
Bao pekee la Simba lilitoka na jitihada za Kibu Denis mpira wake wa kichwa kwenye dakika ya 90 kumparaza Abdallah Heri na kujaa kimiani
Ni matokeo ambayo yanazidi kuiweka Simba katika mazingira magumu kwenye mbio za ubingwa hasa kama watani zao Yanga watashinda mchezo dhidi ya KMC
Alama moja imeirejesha Azam Fc katika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi baada ya kufikisha alama 44 kama ilivyo kwa Singida BS
Azam Fc ina uwiano mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa
Simba imefikisha alama 54 ikisalia nafasi ya pili tofauti ya alama tano dhidi ya Yanga yenye alama 59