Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Ally Mayay amethibitisha kufungwa kwa uwanja wa Benjamin Mkapa kwa ajili ya maboresho
Mayay amesema Shirikisho la soka barani Afrika (CAF) limeagiza kufanyika maboresho makubwa kwa uwanja huo ambao utatumika kwenye michuano ya Africa Super League inayotarajiwa kuanza msimu ujao
Mayay amefafanua kuwa klabu za Simba na Yanga ambazo zinashiriki michuano ya ligi ya mabingwa na kombe la Shirikisho zitaendelea kutumia uwanja huo katika mechi zao za hatua ya makundi
Pia timu ya Taifa 'Taifa Stars' itatumia uwanja katika mechi za kuwania tiketi ya michuano ya Afcon ikitarajiwa kucheza na Uganda mwezi Machi 2023
Uwanja huo hautatumika kwa mechi za ligi kuu, FA ili kupisha maboresho hayo
Uwanja utafunguliwa baada ya awamu ya pili ya ukaguzi wa CAF ambao utafanyika mwezi May 2023