Yanga

Tuko tayari kuikabili Real Bamako - Nabi

Joel JJ By Joel JJ
25 Feb 2023
Tuko tayari kuikabili Real Bamako - Nabi

Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi amesema kikosi chake kiko tayari kwa mchezo wa kombe la Shirikisho dhidi ya Real Bamako ambao utapigwa kesho Jumapili huko Mali

Akizungumza katika Mkutano na Wanahabari mapema leo, Nabi alisema anafahamu ubora wa Real Bamako lakini Yanga imejiandaa vyema, wako tayari kukabiliana nao

"Naifahamu Bamako, ni timu nzuri yenye wachezaji wazoefu, sitegemei utakua mchezo rahisi kwao na kwetu pia, naamini wachezaji wetu wako tayari kupambana kwa dakika 90 za kesho," alisema Nabi

Nabi pia alieleza kuwa na imani na wachezaji wake kuelekea mchezo huu akimtaja mlinda lango Djigui Diarra kama kiongozi atawaongoza wenzake katika mchezo huo hapo kesho

"Diarra ni kipa mzuri mwenye uzoefu mkubwa, ameshathibitisha ubora wake, kuwa naye kwenye kikosi chetu hapa Mali inatupa faida ya kuwa na kiongozi mzuri kwenye safu yetu ya ulinzi"

Akizungumza kwa niaba ya wachezaji wenzake, kiungo mshambuliaji Stephane Aziz Ki alisema wamepata maandalizi mazuri kuelekea mchezo huo hivyo wako tayari kuipambania Yanga

"Tunashukuru uongozi kwa kuweka maandalizi mazuri ya kuhakikisha timu inafanya vizuri, sisi kama wachezaji tuko tayari kwa dakika 90 za kesho"

More Stories

Wamebaki wababe wawili tu wasiofungika Ligi Kuu
Wamebaki wababe wawili tu wasiofungika Ligi Kuu
3h ago
READ MORE →
Afcon haiwezi kuondoka Tanzania, Kenya na Uganda : Motsepe
Afcon haiwezi kuondoka Tanzania, Kenya na Uganda : Motsepe
4h ago
READ MORE →
BREAKING: Tajiri wa Chelsea Boehly ang’atuka kwenye klabu
BREAKING: Tajiri wa Chelsea Boehly ang’atuka kwenye klabu
6h ago
READ MORE →
Ngorongoro Heroes yaweka malengo makubwa CECAFA U20
Ngorongoro Heroes yaweka malengo makubwa CECAFA U20
6h ago
READ MORE →
Yanga SC kukipiga mchezo wa kirafiki na St George uwanja wa Uhuru
Yanga SC kukipiga mchezo wa kirafiki na St George uwanja wa Uhuru
7h ago
READ MORE →
Messi aongeza taji jingine, afikisha mataji 49 katika kazi yake
Messi aongeza taji jingine, afikisha mataji 49 katika kazi yake
7h ago
READ MORE →
Raphinha, Yamal wampa wakati mgumu Mbappe mbio za ufungaji bora La liga
Raphinha, Yamal wampa wakati mgumu Mbappe mbio za ufungaji bora La liga
7h ago
READ MORE →
Manchester United yaanguka Old Trafford, yatupwa nje kwenye Carabao
Manchester United yaanguka Old Trafford, yatupwa nje kwenye Carabao
7h ago
READ MORE →
SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa  Yanga SC “Your next: Yanga”
SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa Yanga SC “Your next: Yanga”
8h ago
READ MORE →
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
10h ago
READ MORE →