Manchester City wanataka kumuongeza kiungo wa kati wa Brighton na Argentina Alexis Mac Allister, 24, kwenye kikosi chao msimu ujao. (Star)
Uwindaji wa Liverpool kumnunua kiungo wa kati wa Borussia Dortmund na England Jude Bellingham hautadhurika na misukosuko yao msimu huu kwani kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa si jambo la kufikia mkataba kwa mchezaji huyo wa miaka 19. (CaughtOffside)
Mshambulizi wa AC Milan na Ufaransa Olivier Giroud yuko tayari kurejea Ligi ya Premia huku klabu za London West Ham, Fulham, Crystal Palace na Brentford zote zikipatikana kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 36. (Sun)
Manchester United wanapanga kumnunua beki wa kulia wa Bayer Leverkusen Mholanzi Jeremie Frimpong, 22. (Football Insider )
Arsenal wameungana na Manchester United katika kinyang'anyiro cha kumnunua kiungo wa kati wa Celta Vigo na Uhispania wa Under-21 Gabri Veiga, 20. (AS, via Sun)
Chelsea itamruhusu kiungo wa kati wa Brazil Andrey Santos, 18, kujiunga na Vasco da Gama kwa mkopo baada ya mkopo uliopendekezwa kwa Palmeiras kushindikana. (Fabrizio Romano)
Newcastle wanafikiria kumnunua kiungo wa Bristol City Muingereza Alex Scott, 19. (Sun) Everton, Leicester, Liverpool, Newcastle, Tottenham, West Ham na Wolves zote zimekuwa zikimfuatilia kiungo wa kati wa Union Berlin Mjerumani Rani Khedira, 29. (90min)
Barcelona na Real Madrid wamefufua nia yao ya kutaka kumnunua kiungo wa kati wa Bayer Leverkusen na Ujerumani Florian Wirtz, huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 19 hivi majuzi akirejea uwanjani baada ya kuumia kwa muda mrefu. (Fijaches - in Spanish)
Burnley wanataka kumbakisha beki wa kulia wa Uholanzi Ian Maatsen, 20, ambaye kwa sasa yuko kwa mkopo kutoka Chelsea, Turf Moor msimu ujao. (Sun)
Chelsea, Barcelona na Real Madrid wanamfuatilia kwa karibu kiungo wa kati wa Inter Milan na Croatia Marcelo Brozovic, 30. (La Gazzetta dello Sport - in Italian)
Kipa wa Sunderland Anthony Patterson, 22, yuko tayari kuitwa kwa kikosi cha Gareth cha England kwa ajili ya kufuzu kwa Euro 2024 mwezi ujao. (Sun)
BBC