Winga wa Misri, Mohamed Salah yuko tayari kuondoka Liverpool msimu wa joto ikiwa klabu hiyo itashindwa kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa msimu ujao. (Fijaches - kwa Kihispania)
Paris St-Germain itakabiliana na ushindani kutoka kwa Liverpool kuwania saini ya mshambuliaji wa AC Milan na Ureno Rafael Leao, huku klabu hiyo ya Merseyside ikiwa tayari kumjumuisha winga wa Colombia Luis Diaz, 26, katika mkataba wa kubadilishana mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23. (Calciomercato - kwa Kiitaliano)
Arsenal wanafanya mazungumzo na 30, kiungo wa kati wa Uswizi Granit Xhaka, kuhusu kuongezwa kwa mkataba mpya wa miaka miwili. (CaughtOffside)
Klabu za Arsenal, Newcastle na West Ham zimetoa ofa ya karibu euro 40m (£35.3m) kumnunua kiungo wa kati wa Lazio na Serbia Sergej Milinkovic-Savic, 27. (Calciomercato - in Italian)
Newcastle wanapanga kumnunua beki wa Arsenal na Scotland Kieran Tierney, 25, msimu wa joto. (Mirror)
Kipa wa Brentford na Uhispania David Raya anasema anataka "kupigania kushinda taji" huku vilabu kadhaa vya Ligi Kuu ya Uingereza, ikiwa ni pamoja na Tottenham vikiwa na nia ya kumsajili. (Atheletic -Usajili unahitajika)
Paris St-Germain wako tayari kuruhusu baadhi ya wachezaji nyota wao kuondoka msimu huu wa joto kwani wanataka kupunguza bili yao ya mishahara kwa asilimia 30. (Times - usajili unahitajika)
Sheikh Jassim bin Hamad Al Thani na Kundi la Ineos la Jim Ratcliffe wangehitaji kuongeza ofa zao za awali ili kuishawishi familia ya Glazer kuiuza Manchester United. (Telegraph - usajili unahitajika)
Nottingham Forest inamfuatilia mlinzi wa Norwich na Jamhuri ya Ireland Andrew Omobamidele, 20. (Sun)
Everton na Bournemouth wanamfuatilia mshambuliaji wa Coventry City na Uswidi Viktor Gyokeres, 24. (Football Insider)
BBC