Maafisa watatu TFF waula CAF

Joel JJ By Joel JJ β€’ 27th February 2023


Maafisa watatu TFF waula CAF

Shirikisho la Soka Barani Afrika 'CAF' limewateuwa Maafisa Watatu kutoka Mamlaka za Soka nchini Tanzania, kuelekea michezo ya Mzunguuko wanne wa Michuano ya Ligi ya mabingwa barani Afrika

Taarifa kutoka CAF imebainisha uteuzi wa Meneja Mashindano wa TFF, Baraka Kizuguto kuwa Mratibu (General Coordinator) wa mchezo wa Hatua ya Makundi Ligi ya Mabingwa Barani Afrika kati ya Mabingwa wa Afrika Kusini Mamelodi Sundowns dhidi ya vs Al Ahly SC ya Misri utakaochezwa Machi 11

Miamba hiyo ilikutana nchini Misri Jumamosi (Februari 25) na mchezo kumalizika kwa matokeo ya sare ya mabao 2-2

Meneja wa Ligi (TPLB), Jonathan Kassano ameteuliwa na CAF kuwa Mratibu (General Coordinator) wa mchezo wa hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Al Hilal (Sudani) vs Mamelodi Sundowns (Afrika Kusini) utakaochezwa Machi 18, 2023.

Mchezo uliopita uliozikutanisha timu hizo katika Uwanja wa Loftus Versfeld mjini Pretoria-Afrika Kusini, Mamelodi Sundowns iliibuka na ushindi wa bao 1-0

Afisa mwingine kutoka TFF aliyeteuliwa na CAF, ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF, Khalid Abdallah ambaye atakuwa Kamishna wa mchezo wa hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika Zamalek SC (Misri) vs E.S.T. (Tunisia) utakaochezwa Machi 7, 2023

Mchezo uliopita wa Mzunguuko watatu ilishuhudiwa Zamalek SC (Misri) ikipigwa 2-0 ugenini katika Uwanja wa Hammadi Agrebi, mjini Tunis-Tunisia.


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.