Transfer

Tetesi za soka Ulaya, Jumanne Februari 28 2023

Joel JJ By Joel JJ
28 Feb 2023
Tetesi za soka Ulaya, Jumanne Februari 28 2023

Chelsea wanafikiria kumrejesha Tammy Abraham katika klabu hiyo kutoka Roma msimu huu wa joto kwani mshambuliaji huyo wa Uingereza mwenye umri wa miaka 25 atakuwa chaguo rahisi kuliko mshambuliaji wa Napoli wa Nigeria Victor Osimhen, 24. (Football Insider)

Mtendaji mkuu wa Inter Milan Giuseppe Marotta anasema mshambuliaji wa Ubelgiji Romelu Lukaku atarejea Chelsea mwishoni mwa msimu wake wa mkopo wa muda mrefu, huku klabu hiyo ya Italia ikiwa bado haijaamua kama wanataka kufanya mazungumzo ya kumnunua mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29. (Sky Sports Italia)

Arsenal itamsajili mshambuliaji wa Chelsea Raheem Sterling ikiwa mshambuliaji huyo wa Uingereza atapatikana msimu wa joto, ingawa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 hataki kuondoka The Blues. (90 Min)

Manchester United wanaamini kuwa wanaweza kumshawishi Declan Rice wa West Ham kujiunga nao msimu wa joto, licha ya kiungo huyo wa kati wa Uingereza mwenye umri wa miaka 24 kutaka kusalia London. (Football Insider)

Ajenti wa mshambuliaji wa Liverpool Mohamed Salah amepuuzilia mbali uvumi kwamba mchezaji huyo wa kimataifa wa Misri mwenye umri wa miaka 30 anaweza kuwahama Reds msimu wa joto ikiwa hawatafuzu kwa Ligi ya Mabingwa. (Goal)

Wasaka vipaji wa Leicester wanafuatilia hali ya kiungo wa kati wa Lecce raia wa Denmark Morten Hjulmand, 23, baada ya Southampton kupata ofa ya euro 11m (£9.7m) iliyokataliwa Januari mwaka jana. (Nicolo Schira)

Manchester City wamewasilisha ombi la kuongeza mkataba wa mshambuliaji wa Argentina Julian Alvarez, 23, hadi mwaka 2028 kwa masharti yaliyoboreshwa. (Fabrizio Romano)

Barcelona ni moja ya vilabu vinavyotathmini kama Alvarez atakuwa tayari kuondoka Manchester City kwa mkopo msimu huu wa joto. (Mundo Deportivo - kwa Kihispania)

Liverpool wanafuatilia kwa karibu mazungumzo ya Chelsea na kiungo wa kati wa Ufaransa N'Golo Kante, 31, kuhusu kuongeza mkataba wake wa sasa, ambao unaisha msimu huu wa joto. (Football Insider)

Paris St-Germain wanajaribu kumshawishimKylian Mbappe, 24, kuchukua kuongeza mkataba wake kwa mwaka mwingine hadi 2025. (L'Equipe, via Sport).

Barcelona na Sergio Busquets wataamua wiki chache zijazo ikiwa kiungo huyo wa zamani wa Uhispania, 34, atasalia na klabu hiyo kwa msimu mwingine. (Sport - kwa Kihispania)

Mkurugenzi wa soka wa Barcelona Mateu Alemany amekataa ofa kutoka kwa Aston Villa kuchukua nafasi kama hiyo katika klabu hiyo ya Ligi Kuu ya Uingereza. (Marca kwa Kihispania)

BBC

More Stories

Afcon haiwezi kuondoka Tanzania, Kenya na Uganda : Motsepe
Afcon haiwezi kuondoka Tanzania, Kenya na Uganda : Motsepe
36m ago
READ MORE →
BREAKING: Tajiri wa Chelsea Boehly ang’atuka kwenye klabu
BREAKING: Tajiri wa Chelsea Boehly ang’atuka kwenye klabu
2h ago
READ MORE →
Ngorongoro Heroes yaweka malengo makubwa CECAFA U20
Ngorongoro Heroes yaweka malengo makubwa CECAFA U20
2h ago
READ MORE →
Yanga SC kukipiga mchezo wa kirafiki na St George uwanja wa Uhuru
Yanga SC kukipiga mchezo wa kirafiki na St George uwanja wa Uhuru
4h ago
READ MORE →
Messi aongeza taji jingine, afikisha mataji 49 katika kazi yake
Messi aongeza taji jingine, afikisha mataji 49 katika kazi yake
4h ago
READ MORE →
Raphinha, Yamal wampa wakati mgumu Mbappe mbio za ufungaji bora La liga
Raphinha, Yamal wampa wakati mgumu Mbappe mbio za ufungaji bora La liga
4h ago
READ MORE →
Manchester United yaanguka Old Trafford, yatupwa nje kwenye Carabao
Manchester United yaanguka Old Trafford, yatupwa nje kwenye Carabao
4h ago
READ MORE →
SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa  Yanga SC “Your next: Yanga”
SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa Yanga SC “Your next: Yanga”
4h ago
READ MORE →
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
6h ago
READ MORE →
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
16h ago
READ MORE →