Yanga

Yanga yatamba kuvuna pesa za Mama Samia

Joel JJ By Joel JJ
β€’
28 Feb 2023
Yanga yatamba kuvuna pesa za Mama Samia

Rais wa Yanga Injinia Hersi Said amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa motisha kwa klabu za Yanga na Simba ili kuhakikisha zinafanya vizuri katika michuano ta CAF wanayoshiriki

Leo Yanga imekabidhiwa Tsh Milioni 5 baada ya kurejea kutoka Mali ambako walicheza na Real Bamako katika mchezo ambao ulimalizika kwa matokeo ya sare ya bao 1-1

Rais wa nchi Dk Samia anatoa motisha ya Tsh Milioni 5 kwa kila goli ambalo linafungwa kwenye michuano ya ligi ya mabingwa na kombe la Shirikisho

Injinia Hersi amesema motisha hiyo imeongeza morali ya ushindani ndani ya timu akisisitiza kuwa hawatarajii kuacha kitu

"Hii ni ishara nzuri kwetu na kwa wachezaji kupambana kwa ajili ya timu na kupata fedha ambazo ni motisha kwao"

"Matokeo ya sare haukuwa mpango wetu tutahakikisha tunapata pointi tatu, matokeo hayo tumeyaacha Mali sasa tumerudi kujipanga na mechi yetu ya Machi nane ambayo wachezaji wameahidi kupata matokeo ya ushindi ikiwa ni pamoja na kufunga idadi kubwa ya mabao ambayo yatamfanya Rais Samia avunje kibubu zaidi," alisema Hersi

Yanga imefunga mabao manne kwenye hatua ya makundi kombe la Shirikisho na hivyo kukusanya Tsh Milioni 20 wakati watani zao Simba wamefunga bao moja lililowapatia Tsh Milioni 5

More Stories

Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
35m ago
READ MORE β†’
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
48m ago
READ MORE β†’
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
1h ago
READ MORE β†’
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
4h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
8h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
8h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
9h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
10h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
10h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
11h ago
READ MORE β†’