Yanga

Yanga yaja na mkakati wa kufuzu robo fainali CAF

Joel JJ By Joel JJ
1 Mar 2023
Yanga yaja na mkakati wa kufuzu robo fainali CAF

Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe amewataka mashabiki wa timu hiyo kuwa tayari kwa mechi mbili za kombe la Shirikisho dhidi ya Real Bamako na US Monastir ambazo zitapigwa uwanja wa Benjamin Mkapa

Kamwe amesema hesabu za Yanga kufuzu robo fainali ya michuano hiyo zimenyooka, wanachopaswa kufanya ni kuhakikisha wanashinda mechi hizo za nyumbani ili kufikisha alama 10

Yanga imetangaza kuzindua kampeni ya kuwahamasisha mashabiki kuujaza uwanja wa Benjamin Mkapa katika mchezo dhidi ya Real Bamako ambao utapigwa Jumatano ijayo, March 08 saa 1 usiku

"Tunahitaji nguvu, hamasa na morali ya mashabiki ili kuhakikisha tunashinda mechi hizi. Safari hii tunataka Benjamin Mkapa iwe imefurika mashabiki wote 60,000. Tunakwenda na slogani hii KWA MKAPA NI FULL SHANGWE"

"Mechi hii tumeikabidhi kwa Wanachama na Mashabiki wa Yanga, tunachohitaji ni shangwe la kutosha kutoka kwa mashabiki ili kuwapa hamasa wachezaji wetu zaidi ya vile tulivyofanya katika mchezo dhidi ya TP Mazembe," alisema Kamwe

Kampeni ya hamasa kuelekea mchezo dhidi ya Real Bamako itazinduliwa kesho Alhamisi, Buruguni (Chama) jijini Dar es salaam. Tiketi za mchezo huo zitaanza kuuzwa leo

Viingilio Mzunguuko ni Tsh 3,000/- VIP C ni Tsh 10,000/-, VIP B ni Tsh 15,000/- na VIP A ni Tsh 20,000/-

More Stories

Wamebaki wababe wawili tu wasiofungika Ligi Kuu
Wamebaki wababe wawili tu wasiofungika Ligi Kuu
3h ago
READ MORE →
Afcon haiwezi kuondoka Tanzania, Kenya na Uganda : Motsepe
Afcon haiwezi kuondoka Tanzania, Kenya na Uganda : Motsepe
4h ago
READ MORE →
BREAKING: Tajiri wa Chelsea Boehly ang’atuka kwenye klabu
BREAKING: Tajiri wa Chelsea Boehly ang’atuka kwenye klabu
6h ago
READ MORE →
Ngorongoro Heroes yaweka malengo makubwa CECAFA U20
Ngorongoro Heroes yaweka malengo makubwa CECAFA U20
6h ago
READ MORE →
Yanga SC kukipiga mchezo wa kirafiki na St George uwanja wa Uhuru
Yanga SC kukipiga mchezo wa kirafiki na St George uwanja wa Uhuru
7h ago
READ MORE →
Messi aongeza taji jingine, afikisha mataji 49 katika kazi yake
Messi aongeza taji jingine, afikisha mataji 49 katika kazi yake
7h ago
READ MORE →
Raphinha, Yamal wampa wakati mgumu Mbappe mbio za ufungaji bora La liga
Raphinha, Yamal wampa wakati mgumu Mbappe mbio za ufungaji bora La liga
7h ago
READ MORE →
Manchester United yaanguka Old Trafford, yatupwa nje kwenye Carabao
Manchester United yaanguka Old Trafford, yatupwa nje kwenye Carabao
7h ago
READ MORE →
SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa  Yanga SC “Your next: Yanga”
SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa Yanga SC “Your next: Yanga”
8h ago
READ MORE →
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
10h ago
READ MORE →