Real Madrid - Barcelona

Real Madrid uso kwa na Barcelona nusu fainali Copa del Rey

Joel JJ By Joel JJ
β€’
2 Mar 2023
Real Madrid uso kwa na Barcelona nusu fainali Copa del Rey

Mabingwa wa Ulaya Real Madrid leo majira ya saa 5 usiku watakuwa wenyeji wa vinara wa La Liga FC Barcelona katika mkondo wa kwanza wa nusu fainali ya Copa del Rey Uwanja wa Santiago Bernebeu

Michuano hiyo lililoanzishwa mwaka wa 1903, ni mojawapo ya mashindano ya zamani zaidi ya soka ya Hispania

Barcelona inaongoza kwa kutwaa mataji ya Copa del Rey ikishinda mataji 19 waati Real Madrid inashika nafasi ya tatu

Real Madrid na Barcelona zilijikatia tiketi ya kutinga nusu fainali kwa kuzishinda Atletico Madrid na Real Sociedad

Real Madrid ilitinga nusu fainali baada ya kuwachapa majirani zao Atletico Madrid mabao 3-1, wakati Fc Barcelona waliwafunga Real Sociedad 1-0 katika mchezo wa robo fainali

Wakati meneja wa Real Madrid Carlo Ancelotti akitarajiwa kuchezesha kikosi chake kamili, meneja wa Barcelona Xavi Hernandez anaweza kuwakosa baadhi ya wachezaji wake nyota.

Ousmane Dembele na kiungo wa kati wa Barca wa Uhispania Pedri ni majeruhi na hawatakuwa sehemu ya mechi hiyo.

Nyota wa Poland Robert Lewandowski pia huenda akakosekana kutokana na jeraha la misuli ya paja

Pia itakuwa ni mechi ya pili kati ya Real Madrid dhidi ya Barcelona mwaka huu. Katika fainali ya Super Cup 2022-23 mnamo Januari, Barcelona ilishinda Real Madrid 3-1, shukrani kwa mabao ya Gavi, Robert Lewandowski na Pedri.

Mechi nyingine za nusu fainali kwenye Copa del Rey ni kati ya Osasuna dhidi ya Athletic Bilbao.

More Stories

Mizzima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizzima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
3h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
7h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
7h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
8h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
9h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
9h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
10h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
10h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
1d ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
1d ago
READ MORE β†’