Transfer

Tetesi za soka Ulaya, Ijumaa March 03 2023

Joel JJ By Joel JJ
3 Mar 2023
Tetesi za soka Ulaya, Ijumaa March 03 2023

Liverpool watakuwa mstari wa mbele katika kinyang'anyiro cha kumsajili kiungo wa kati wa Chelsea na Uingereza Mason Mount msimu huu wa joto, ikiwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 hataweza kuafiki mkataba mpya Stamford Bridge. (Mail)

Real Madrid itatathmini mustakabali wa muda mrefu wa Mkroatia Luka Modric, 37, na Mjerumani na kiungo mwenza Toni Kroos kabla ya kujitolea kuhamia England nae kiungo wa kati wa Borussia Dortmund Jude Bellingham, 19, ambaye ameambiwa akate kuhamia Liverpool. (Diario AS - kwa Kihispania)

Real Madrid pia wanamfuatilia kiungo wa kati wa Newcastle Mbrazil Bruno Guimaraes, 25, kwa muda uliosalia wa msimu wa 2022-23 kama chaguo mbadala kwa Bellingham. (Mundo Deportivo - kwa Kihispania)

Chelsea wamefufua nia yao ya kumnunua mlinzi wa RB Leipzig Josko Gvardiol, 21, huku Manchester City na Tottenham pia wakimtaka mchezaji huyo wa kimataifa wa Croatia ambaye ana kipengele cha kumuachia cha pauni milioni 97 katika mkataba wake utakaoanza kutekelezwa kuanzia 2024. (Times).

Inter Milan wanatumai kumsajili Naby Keita, 28, msimu huu wa joto wakati mkataba wa kiungo huyo wa kati wa Guinea utakapomalizika Liverpool na tayari wamefanya mazungumzo ya kutia moyo na wawakilishi wake. (Gazzetta dello Sport - kwa Kiitaliano)

Kiungo wa kati wa Lyon Mfaransa Houssem Aouar, 24, anakaribia kusaini Eintracht Frankfurt kwa uhamisho wa bila malipo baada ya kukataa kuhamia Manchester United. (Sport1)

Barcelona wanaweza kuwauza baadhi ya nyota wao wakubwa huku klabu hiyo yenye matatizo ya kifedha ikitafuta kuongeza pauni milioni 178, huku winga wa Brazil Raphinha, 26, akiwa miongoni mwa wale ambao wanaweza kuondolewa. (Sun)

Manchester United wameungana na Chelsea na Arsenal kumfuatilia kiungo wa kati wa Southampton raia wa Ubelgiji Romeo Lavia, 19. (Mail)

Tottenham wanatazamia kumnunua kiungo wa Bristol City Alex Scott majira ya kiangazi. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza mwenye umri wa miaka 19 pia anavutia Crystal Palace na West Ham. (Sun)

Leicester na Everton wanamfuatilia kiungo wa kati wa Bologna na Scotland Lewis Ferguson, 23. (Nicolo Schira)

Nottingham Forest wanakabiliwa na pambano la kutaka kumbakisha kocha Steve Cooper msimu ujao huku vilabu kadhaa vya Premier League vikiwa vimevutiwa na meneja huyo. (Mail)

Mazungumzo yanaendelea kati ya Manchester United na David de Gea. Kipa huyo wa Uhispania, 32, mkataba wake unamalizika msimu wa joto, lakini anatamani kusalia Old Trafford. (Fabrizio Romano)

Manchester United wamepokea maombi ya mkopo kutoka kwa vilabu nchini Uturuki kwa ajili ya mshambuliaji wao wa Uingereza Mason Greenwood, 21, ambaye bado amesimamishwa na klabu hiyo licha ya mashtaka ya uhalifu dhidi yake kutupiliwa mbali mwezi Februari. (Telegraph)

Napoli inasalia na uhakika wa kumbakisha winga wa Georgia Khvicha Kvaratskhelia, 22, licha ya Manchester City, Chelsea, Real Madrid na Barcelona kumtaka winga huyo. (90 min)

Fulham wanataka kufanya uhamisho wa mkopo wa winga wa Israel Manor Solomon mwenye umri wa miaka 23 kutoka Shakhtar Donetsk kuwa wa kudumu msimu huu. (Normal)

BBC

More Stories

BREAKING: Tajiri wa Chelsea Boehly ang’atuka kwenye klabu
BREAKING: Tajiri wa Chelsea Boehly ang’atuka kwenye klabu
56m ago
READ MORE →
Ngorongoro Heroes yaweka malengo makubwa CECAFA U20
Ngorongoro Heroes yaweka malengo makubwa CECAFA U20
1h ago
READ MORE →
Yanga SC kukipiga mchezo wa kirafiki na St George uwanja wa Uhuru
Yanga SC kukipiga mchezo wa kirafiki na St George uwanja wa Uhuru
2h ago
READ MORE →
Messi aongeza taji jingine, afikisha mataji 49 katika kazi yake
Messi aongeza taji jingine, afikisha mataji 49 katika kazi yake
2h ago
READ MORE →
Raphinha, Yamal wampa wakati mgumu Mbappe mbio za ufungaji bora La liga
Raphinha, Yamal wampa wakati mgumu Mbappe mbio za ufungaji bora La liga
2h ago
READ MORE →
Manchester United yaanguka Old Trafford, yatupwa nje kwenye Carabao
Manchester United yaanguka Old Trafford, yatupwa nje kwenye Carabao
2h ago
READ MORE →
SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa  Yanga SC “Your next: Yanga”
SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa Yanga SC “Your next: Yanga”
3h ago
READ MORE →
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
4h ago
READ MORE →
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
15h ago
READ MORE →
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
15h ago
READ MORE →