Msafara wa timu ya Real Bamako umewasili Dar kuelekea mchezo wa kombe la Shirikisho dhidi ya Yanga ambao utapigwa Jumatano, March 08 katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Bamako wametua usiku wa kuamkia leo huku wakitamba kuwa wamekuja kuishangaza Yanga
Katika mchezo wa kwanza uliopigwa Mali wiki iliyopita, ulimalizika kwa matokeo ya sare ya bao 1-1
Matokeo hayo yaliendelea kuiweka Yanga kwenye nafasi ya pili katika msimamo wa kundi D ikiwa na alama nne
Real Bamako wako mkiani wakiwa na alama mbili ambazo zote walizipata kwenye uwanja wao wa nyumbani kwa kulazimishwa sare dhidi ya US Monastir na Yanga
TP Mazembe wanashika nafasi ya tatu wakiwa na alama tatu wakati US Monastir wanaongoza kundi wakiwa na alama saba
Wakati Yanga ikichuana na Real Bamako Dar, US Monastir watakuwa wakichuana na TP Mazembe huko Tunisia
Kama Yanga itashinda na TP Mazembe kupoteza, basi Yanga itahitaji kushinda mchezo utakaofuata dhidi ya US Monastrir ili kutinga robo fainali