Liverpool - Manchester United

Klopp aihofia Manchester United

Joel JJ By Joel JJ
β€’
5 Mar 2023
Klopp aihofia Manchester United

Bosi wa Liverpool, Jurgen Klopp, amefunguka kuwa, ni lazima wajipange dhidi ya Manchester United kwani kwenye kikosi cha wapinzani wao wana wachezaji wengi bora

Leo Jumapili, Liverpool itavaana na Manchester United katika mchezo wa wa Premier League mzunguko wa pili ukitarajiwa kuchezwa Uwanja wa Anfield

Katika mchezo wa awali ambao Manchester United walikuwa nyumbani Old Trafford, waliibuka na ushindi wa mabao 2-1.

Pamoja na Marcus Rashford kuonekana ndiye mchezaji hatari zaidi ndani ya kikosi cha United, Klopp amesema sio yeye pekee

"Rashford ana uwezo wa kufunga na anafunga mabao rahisi sana, anafanya mambo mazuri uwanjani na anajua namna ya kujilinda. Lakini yeye sio mchezaji pekee wa daraja la juu ndani ya Man United, hivyo tunahitaji umakini mkubwa"

"Kuna mchezaji kama Bruno (Fernandes), napenda namna anavyocheza, akiwa na mpira yupo smati, unaweza kushangaa huyu hapa tu"

"Casemiro na Fred hawa wakichezaji pamoja wanakuwa bora hasa kwa kulinda, kifiziki wako vizuri na wana uwezo wa kufanya mashambulizi ya kushitukiza kama ilivyo kwa Sancho (Jadon) ndiyo maana tunatakiwa kuwa makini na Man United"

"Lakini pia mchezo huu utakuwa mgumu japo wapinzani wetu wanatakiwa kujua matokeo hayahusiani na masuala ya top four, zaidi hapa tunahitaji ushindi," alisema Klopp

Liverpool hawakuwa na mwenendo mzuri msimu huu lakini matokeo ya ushindi dhidi ya Man United leo yatafufua matumaini yao ya kumaliza katika nafasi nne za juu

More Stories

Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
8h ago
READ MORE β†’
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
8h ago
READ MORE β†’
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
9h ago
READ MORE β†’
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
12h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
16h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
16h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
17h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
17h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
18h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
19h ago
READ MORE β†’