Simba - Yanga - Azam - Taifa Stars - Tanzania

Ukarabati dimba la Mkapa kufanyika kwa awamu tatu

Joel JJ By Joel JJ
β€’
5 Mar 2023
Ukarabati dimba la Mkapa kufanyika kwa awamu tatu

Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo imeanza kutekeleza maagizo ya Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa pamoja na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) ya kuanza ukarabati wa Uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es Salaam

Akizungumza wakati wa ziara ya kujipanga kutekeleza maagizo hayo, Machi 5, 2023 Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Ndg. Saidi Yakubu amesema ukarabati huo utaanza mara baada ya mshauri mwelekezi kukamilisha kazi yake

"Ukarabati huu utakua na awamu tatu, ya kwanza itakua ni ukarabati katika maeneo ya kubadilishia nguo, maliwato, kurekebisha viti vilivyoharibika, kuongeza taa ndani ya uwanja na maeneo mengine"

"Pia kukarabati mfumo wa umeme na maji pamoja na eneo la waandishi wa habari ambapo tutawahamisha wanapokaa hivi sasa na kuwatengea eneo zuri zaidi" amesema Yakubu.

"Awamu ya pili itakua ni ukarabati mkubwa ambao utatekelezwa na wakandarasi wa kimataifa na utahusisha eneo la kuchezea (pitch) kupanua sehemu ya watu mashuhuri, kuweka televisheni kubwa yenye muonekano ang'aavu"

Katibu Mkuu Yakubu ameongeza kuwa awamu ya tatu itahusisha kupanua uwanja pamoja na kujenga viwanja vingine vidogo ikiwemo vya kuogelea katika eneo lililobaki, kuweka viti vya kisasa, kutenga eneo la kupumzika watu mashuhuri na kuufanya uwe kivutio kwa jiji la Dar es Salaam

Ukarabati huo utafanyika chini ya Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) kama mshauri mwelekezi

More Stories

Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
6h ago
READ MORE β†’
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
6h ago
READ MORE β†’
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
7h ago
READ MORE β†’
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
10h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
14h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
14h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
15h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
16h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
16h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
17h ago
READ MORE β†’