SImba

Simba yanusa robo fainali Ligi ya Mabingwa

Joel JJ By Joel JJ
7 Mar 2023
Simba yanusa robo fainali Ligi ya Mabingwa

Wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika Simba, leo wametakata uwanja wa Benjamin Mkapa wakiibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Vipers Fc

Bao pekee la ushindi kwa Simba iliyotawala mchezo huo kwa muda mwingi lilifungwa na Clatous Chama kwenye dakika ya 45

Ni ushindi muhimu kwa Simba ambao umewasogeza kwenye nafasi ya pili kundi C baada ya kufikisha alama sita

Wapinzani wao wa karibu Horoya Ac wamekubali kipigo cha mabao 3-1 kutoka kwa Raja Casablanca iliyojihakikishia kutinga robo fainali baada ya ushindi huo

Horoya wameshuka nafasi ya tatu katika kundi C wakibaki na alama zao nne

Simba imenusa hatua ya robo fainali kwani sasa inahitaji kushinda mchezo unaofuata dhidi ya Vipers Fc ambao utapigwa uwanja wa Benjamin Mkapa ili kukata tiketi kabla ya mchezo wao wa mwisho dhidi ya Raja Casablanca utakaopigwa huko Morocco

More Stories

Yanga SC kukipiga mchezo wa kirafiki na St George uwanja wa uhuru
Yanga SC kukipiga mchezo wa kirafiki na St George uwanja wa uhuru
52m ago
READ MORE →
Messi aongeza taji jingine, afikisha mataji 49 katika kazi yake
Messi aongeza taji jingine, afikisha mataji 49 katika kazi yake
55m ago
READ MORE →
Raphinha, Yamal wampa wakati mgumu Mbappe mbio za ufungaji bora La liga
Raphinha, Yamal wampa wakati mgumu Mbappe mbio za ufungaji bora La liga
1h ago
READ MORE →
Manchester United yaanguka Old Trafford, yatupwa nje kwenye Carabao
Manchester United yaanguka Old Trafford, yatupwa nje kwenye Carabao
1h ago
READ MORE →
SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa  Yanga SC “Your next: Yanga”
SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa Yanga SC “Your next: Yanga”
1h ago
READ MORE →
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
3h ago
READ MORE →
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
13h ago
READ MORE →
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
13h ago
READ MORE →
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
14h ago
READ MORE →
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
17h ago
READ MORE →