Yanga

Yanga yaichapa Real Bamako 2-0

Joel JJ By Joel JJ
β€’
8 Mar 2023
Yanga yaichapa Real Bamako 2-0

Yanga imetakata uwanja wa Benjamin Mkapa jioni hii wakiibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Real Bamako katika mchezo wa kombe la Shirikisho

Mabao ya Fiston Mayele na Jesus Moloko yaliihakikishia Yanga alama tatu muhimu ambazo zimewaweka katika nafasi nzuri ya kutinga robo fainali ya michuano hiyo

Bao la kwanza la Yanga lilifungwa na Mayele kwenye dakika ya 8 akimalizia shambulizi lililoanzishwa na Kennedy Musonda

Mayele angeweza kufunga hata mabao matatu kwenye kipindi cha kwanza kama angeongeza umakini

Wakati wa mapumziko kocha Nasreddine Nabi alifanya mabadiliko muhimu akiboresha eneo la kiungo akimuingiza Khalid Aucho nafasi ya Aziz Ki huku Jesus Moloko akiingia nafasi ya Tuisila Kisinda aliyeumia

Mabadiliko hayo yaliiongezea Yanga ubora na kutengeneza nafasi zaidi ikiwemo mkwaju wa penati baada ya Mayele kufanyiwa madhambi katika eneo la hatari

Yannick Bangala alikosa mkwaju huo lakini kwenye dakika ya 68 Moloko akafunga bao la pili baada ya kumnyang'anya mpira mlinzi wa Bamako

Ni ushindi ambao umeifanya Yanga ifikishe alama saba na kujiimarisha katika nafasi ya pili

Yanga inahitaji kushinda mchezo dhidi ya US Monastir ili kufuzu hatua ya robo fainali

Mapema TP Mazembe ilikubali kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa US Monastir sasa ikisalia nafasi ya tatu ikiwa na alama tatu

More Stories

Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
1h ago
READ MORE β†’
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
11h ago
READ MORE β†’
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
11h ago
READ MORE β†’
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
11h ago
READ MORE β†’
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
15h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
18h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
19h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
20h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
20h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
21h ago
READ MORE β†’