Transfer

Tetesi za soka Ulaya, Alhamisi March 09 2023

Joel JJ By Joel JJ
β€’
9 Mar 2023
Tetesi za soka Ulaya, Alhamisi March 09 2023

Manchester United wako tayari kutoa euro 130m (£115m) kumsajili kiungo wa kati wa Ufaransa Eduardo Camavinga, 20, kutoka Real Madrid. (Fichajes – in Spanish)

Mshambulizi wa Tottenham na England Harry Kane, 29, yuko kwenye orodha ya usajili ya meneja wa Manchester United Erik ten Hag, kama ilivyo kwa kiungo mshambuliaji wa Ghana Mohammed Kudus, 22 kutoka klabu ya zamani ya Mholanzi huyo Ajax. (TalkSport)

Lakini United watataka kuwauza wachezaji kadhaa wa kikosi cha kwanza, akiwemo beki wa Uingereza Harry Maguire, 30, ili kutoa nafasi kwa wachezaji wapya msimu huu wa joto. (ESPN)

Borussia Dortmund haitaondoa thamani yao ya euro 150m (£133m) ya kiungo wa kati wa Uingereza Jude Bellingham mwenye umri wa miaka 19 huku Liverpool, Manchester City na Real Madrid zikimtaka. (90 min)

Liverpool wanazidi kujiamini kwamba watashinda mbio za kuinasa saini ya Bellingham lakini matumaini yao ya kufanya hivyo huenda yakaegemea kwenye jitihada zao za kushiriki soka la Ligi ya Mabingwa. (Mail)

Paris St-Germain wana nia ya kumsajili beki wa Newcastle United Mholanzi Sven Botman mwenye umri wa miaka 23. (iNews)

Mlinzi wa Leeds United Mjerumani Robin Koch, 26, anazingatiwa kama mchezaji anayetarajiwa kusajiliwa na Newcastle United, ingawa vilabu kadhaa vya Bundesliga pia vinavutiwa. (Sport1 – In Germany)

Mshambuliaji wa Ubelgiji Eden Hazard, 32, ananuia kusalia Real Madrid hadi kandarasi yake itakapokamilika 2024. (Athletic)

Bayern Munich watakataa nafasi ya kufanya usajili wa mkopo wa beki wa pembeni wa Manchester City Joao Cancelo, 28, wa kudumu kwa £62m. ( Calciomercato, Via Mail )

Newcastle United inaweza kuwashawishi Barcelona kumuuza winga wa Brazil Raphinha, 26, ikiwa wanaweza kufikia ada ya £55m ambayo klabu ya Uhispania ililipa kumsajili kutoka Leeds United mwaka jana. (El Desmarque)

Liverpool wanaongoza katika kinyang'anyiro cha kumsajili mchezaji wa kimataifa wa Uingereza Mason Mount, 24, kutoka Chelsea na Mreno Matheus Nunes, 24, kutoka Wolves huku Jurgen Klopp akijaribu kurekebisha safu yake ya mshambulizi. (Mail)

Mlinda mlango wa Brentford David Raya anatarajiwa kuondoka katika klabu hiyo ya Ligi ya Premia msimu wa joto baada ya kukataa ofa mbili za kandarasi mpya. Mhispania huyo mwenye umri wa miaka 27, ambaye mkataba wake unamalizika 2024, amekuwa akihusishwa na Chelsea na Tottenham. (Fabrizio Romano)

Meneja wa Chelsea Graham Potter alishawishi ushindi mara mbili dhidi ya Leeds United na Borussia Dortmund ambao uliokoa kibarua chake kwa kufanya mazungumzo ya moyo kwa moyo na wachezaji wake. (Telegraph)

Aston Villa wanataka kumsajili mlinzi wa Athletic Bilbao Muhispania Inigo Martinez kwa uhamisho wa bila malipo msimu wa joto, lakini wanakabiliwa na ushindani kutoka kwa Barcelona na Atletico Madrid kumnunua mchezaji huyo wa miaka 31 aliye nje ya mkataba. (Mail in Birmingham)

BBC

More Stories

Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
35m ago
READ MORE β†’
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
48m ago
READ MORE β†’
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
1h ago
READ MORE β†’
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
4h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
8h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
8h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
9h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
10h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
10h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
11h ago
READ MORE β†’