Ruvu - Mbeya City

Ruvu Shooting ni kufa au kupona Ligi Kuu

Joel JJ By Joel JJ
10 Mar 2023
Ruvu Shooting ni kufa au kupona Ligi Kuu

Wakati leo inashuka ugenini kuwakabili Mbeya City katika mechi ya Ligi Kuu Bara itakayochezwa kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya, Ruvu Shooting imetangaza hali ya hatari katika mechi zake sita zilizobaki

Msemaji wa Ruvu Shooting, Masau Bwire, alisema mechi hizo ni za ukombozi kwa timu yao inayoburuza mkia na ahadi ya kupata matokeo chanya wanaianza leo watakapowavaa Mbeya City.

"Kikosi kiko jijini Mbeya muda mrefu, kiko huko kwa shughuli maalum ya kuhakikisha hizi mechi tulizosalia nazo zinaleta ukombozi kwenye klabu yetu, kwa hiyo ni lazima tujidhatiti, tujiweke vizuri ili tukae eneo salama, tuliwahi kwa lengo la kusoma mazingira yasije yakawaathiri vijana watapokuwa uwanjani wakiitetea timu yao," alisema Bwire

Alisema wameandaa mpango maalum wa kiufundi wa kuhakikisha timu hiyo haishuki daraja kwa kuimarisha umoja kuanzia kwa wachezaji, benchi la ufundi na viongozi wa timu hiyo.

Ruvu Shooting yenye pointi 17 imecheza mechi 24 na kati ya hizo imeshinda michezo minne, sare tano na kupoteza michezo 15.

More Stories

Yanga SC kukipiga mchezo wa kirafiki na St George uwanja wa uhuru
Yanga SC kukipiga mchezo wa kirafiki na St George uwanja wa uhuru
52m ago
READ MORE →
Messi aongeza taji jingine, afikisha mataji 49 katika kazi yake
Messi aongeza taji jingine, afikisha mataji 49 katika kazi yake
56m ago
READ MORE →
Raphinha, Yamal wampa wakati mgumu Mbappe mbio za ufungaji bora La liga
Raphinha, Yamal wampa wakati mgumu Mbappe mbio za ufungaji bora La liga
1h ago
READ MORE →
Manchester United yaanguka Old Trafford, yatupwa nje kwenye Carabao
Manchester United yaanguka Old Trafford, yatupwa nje kwenye Carabao
1h ago
READ MORE →
SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa  Yanga SC “Your next: Yanga”
SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa Yanga SC “Your next: Yanga”
1h ago
READ MORE →
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
3h ago
READ MORE →
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
13h ago
READ MORE →
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
13h ago
READ MORE →
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
14h ago
READ MORE →
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
17h ago
READ MORE →