Real Madrid wamepata ushindi wao wa kwanza wa La Liga baada ya mechi tatu walipotoka nyuma na kuifunga Espanyol mabao 3-1
Espanyol walianza vyema Joselu akiwaweka mbele wasumbufu hao kutoka Catalan baada ya dakika nane.
Lakini mabao kutoka kwa Vinicius Jr na Eder Militao yaliipa Real Madrid uongozi na kuhakikisha ushindi kwa bao la dakika za mwisho la Marco Asensio
Real Madrid ambayo iko pointi sita nyuma ya Barcelona iliyoko kileleni huku Real Madrid wakiwa wamecheza mechi moja zaidi, watamenyana na Barca kwenye El Clasico wikendi ijayo.



