Transfer

Tetesi za soka Ulaya, Jumapili March 12 2023

Joel JJ By Joel JJ
β€’
12 Mar 2023
Tetesi za soka Ulaya, Jumapili March 12 2023

Klabu ya Manchester United inajipanga kumfanya Harry Kane, 29, kuwa mchezaji ghali zaidi wa Uingereza katika historia kwa kumsajjili kutka Tottenham mwishoni mwa msimu. (Mirror)

Manchester United wakati huohuo inahofu kuwa itashindwa kumuuza nahodha wake na mlinzi wa kati wa England Harry Maguire, 30, mwishoni mwa msimu huu kutokana ukubwa wa mshahara wake ambao inaaminika kuwa umevuka pauni 200,000 kwa wiki. (Football Insider)

Paris St-Germain inaweza kupeleka ofa ya kumsajili mshambuliaji nyota wa Norway Erling Haaland, 22, kutoka Manchester City na kumuunganisha na mshambuliaji nyota wa Ufaransa Kylian Mbappe, 24. (RMC Sport, via Sport - in Spanish)

Mipango ya kocha wa United Ten Hag katika dirisha la usajili la mwishoni mwa msimu haijabadilika hata baada ya kufungwa 7-0 na Liverpool. (Telegraph - subscription required);

Chelsea wamemfanya kiungo nyota wa Uholanzi na klabu ya Barcelona Frenkie de Jong, 25, kuwa mchezaji wa kipumbele katika dirisha la usajili la mwishoni mwa msimu. (Football Insider)

Mshambuliajji wa Ureno Joao Felix, 23, anafurahia muda wake wa mkopo katika klabu ya Chelsea na anatarajiwa kufanya mazungumzo na klabu yake ya Atletico Madrid juu ya uwezekano wa kuihama moja kwa moja mwishoni mwa msimu. (Relevo)

Koch awa zamani wa Aston Villa Steven Gerrard amesafiri kuelekea Istanbul kufanya mazungumzo na klabu ya Trabzonspor ili kuwa kocha wake mkuu. (Karar - in Turkish)

Tottenham wanataka kumsajili kipa namba moja wa England Jordan Pickford, 29, mwishoni mwa msimu licha ya nyanda huyo kusaini mkataba wa muda mrefu na klabu yake ya Everton. (Sun)

Barcelona haitazamiwi kuendelea na harakati za kutaka kumsajili kiungo mshambuliaji wa Ureno Bernardo Silva, 28, kwakuwa klabu yake ya Manchester City itataka kulipwa wastani wa pauni milioni 70 ili imuuze. (Mundo Deportivo - in Spanish)

Manchester City wapo ukingoni kufikia makubaliano mapya na mshambuliaji wa Argentina Julian Alvarez, 23, ambayo yatarefusha mkataba wake mpaka mwaka 2028 na kumpa nyongeza maradufu ya mshahara. (TyC Sports - in Spanish)

Matakwa ya mshahara ya Naby Keita, 28, yameifanya klabu ya AC Milan kujiondoa katika mbio za kumsajili kiungo huyo wa Guinea ambaye atakuwa mchezaji huru mwishoni mwa msimu ambapo mkataba wake na Liverpool utakapofikia tamati. (Calciomercato - in Italian)

Klabu ya Marekani ya St Louis City ni moja kati ya vilabu vinavyomwania mshambuliaji wa Brazil na Roberto Firmino, 31, ambaye pia atakuwa mchezaji huru mkataba wake na Liverpool utakapokoma mwishoni mwa msimu huu. (Bleacher Report)

BBC

More Stories

Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
3h ago
READ MORE β†’
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
3h ago
READ MORE β†’
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
3h ago
READ MORE β†’
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
7h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
10h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
11h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
12h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
12h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
13h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
14h ago
READ MORE β†’