Polisi Tanzania

Hatutashuka daraja - Zahera

Joel JJ By Joel JJ
β€’
13 Mar 2023
Hatutashuka daraja - Zahera

Licha ya kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa Dodoma Jiji hapo jana, Kocha Mkuu wa Polisi Tanzania Mwinyi Zahera amesisitiza kuwa haoni timu yake ikiteremka daraja

Polisi Tanzania inashika nafasi ya 16 (mwisho) kwenye msimamo wa ligi wakiwa na alama 19 huku timu hiyo ikiwa imesalia na mechi tano

Zahera amesema anaamini katika mechi zilizosalia bado wana nafasi ya kupambana ili wabaki Ligi Kuu

"Sijafikiria hata siku moja kwamba timu itashuka daraja! Bado zimebaki mechi tano (5) ambazo ni sawa na alama 15"

"Ikifika wakati hata tukishinda alama zitakuwa hazitusaidii kitu tunaweza kuamini tumeshuka lakini kwa sasa bado sifikirii kama hii timu itashuka," alisema Zahera baada ya kipigi cha mabao 2-1 kutoka kwa Dodoma Jiji katika mchezo uliopigwa uwanja wa Jamhuri

Polisi Tanzania wana alama 19, Ruvu Shooting ipo juu yake ikiwa na alama 20. Kwenye eneo la kucheza play offs kuna Coastal Union alama 26 na Tanzania Prisons alama 25 ambazo zinaweza kufikiwa na Polisi Tanzania

Polisi Tanzania inaweza kutoka chini hadi kwenye eneo salama ambalo ni nafasi ya tisa (9) hadi 12 ambako anaweza kuzifikia alama za timu zilizopo eneo hilo

Polisi Tanzania imebakiza mechi dhidi ya Singida Big Stars (A) Ihefu (H), Mtibwa Sugar (H), Azam (A) na Simba (A).

More Stories

Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
8h ago
READ MORE β†’
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
8h ago
READ MORE β†’
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
8h ago
READ MORE β†’
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
12h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
15h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
16h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
16h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
17h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
18h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
19h ago
READ MORE β†’