Barcelona - Manchester United

Xavi apigilia msumari kuhusu De Jong

Joel JJ By Joel JJ
β€’
13 Mar 2023
Xavi apigilia msumari kuhusu De Jong

Kocha Mkuu wa Fc Barcelona Xavi Fernandez ameeleza kuvutiwa na kiwango cha kiungo Frank De Jong akieleza timu yake inafurahia huduma yake

De Jong anawindwa na Manchester United tangu dirisha la usajili la majira ya joto hata hivyo kiungo huyo ameweka msimamo hana mpango wa kundoka Fc Barcelona

Kocha wa Manchester United Erik Ten Hag anamuhitaji sana De Jong katika kikosi chake, akiwa mmoja wa wachezaji aliopata nao mafanikio wakati yuko Ajax ambapo msimu wa 2019-20 walitinga nusu fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya

"Frenkie de Jong ni mmoja wa viungo bora zaidi duniani kwa sasa, yuko kwenye kiwango cha kuvutia, anacheza kwa kiwango cha ajabu anatupa mengi, nina furaha sana na Frenkie,"alisema Xavi

Jana De Jong alikuwa sehemu ya kikosi cha Barcelona kilichopata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Athletic Club na kuendelea kujikita kileleni mwa msimamo wa La Liga kwa tofauti ya alama tisa dhidi ya wapinzani wao Real Madrid

Fc Barcelona wana alama 65 wakati Real Madrid wana alama 56 timu hizo zikitarajiwa kuchuana katika mchezo wa El Classico mwishoni mwa wiki

More Stories

Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
7h ago
READ MORE β†’
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
7h ago
READ MORE β†’
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
8h ago
READ MORE β†’
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
11h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
14h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
15h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
16h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
16h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
17h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
18h ago
READ MORE β†’