Tutaleta taji la CAF Tanzania - Hersi

Joel JJ By Joel JJ β€’ 16th March 2023


Tutaleta taji la CAF Tanzania - Hersi

Rais wa Yanga Injinia Hersi Said amesema ana imani kubwa kuwa wana nafasi nzuri ya kuendelea kufanya vizuri katika michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika Yanga ikishika nafasi ya pili kundi D

Yanga inahitaji kushinda mchezo unaofuata dhidi ya US Monastir ambao utapigwa Jumapili, March 19 ili kutinga robo fainali ya michuano hiyo

Hersi amesema kama watafanikiwa kutinga robo fainali, wanaweza kusonga mbele hatua ya nusu fainali, na hata kwenda mbali zaidi hatua ya fainali na hata kutwaa ubingwa

Hersi amesema anaamini Yanga itakuwa timu ya kwanza kutoka Tanzania kutwaa taji la CAF;

"Sisi ndio tutakuwa timu ya Kwanza kutoka kwenye ardhi ya Tanzania kulileta Kombe la CAF nchini. Inshallah Jumapili tukifanikiwa kutinga Robo fainali nina Imani tutavuka na kwenda Nusu fainali, baadae Fainali na Inshallah sisi ndio itakuwa timu ya Kwanza kushangilia taji hili"

"Wananchi msiwe na hofu Inshallah sisi mwaka huu tutalibeba," alitamba Hersi


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.