Borussia Dortmund - Ivory Coast

Haller ajumuishwa timu ya Taifa Ivory Coast

Joel JJ By Joel JJ
β€’
16 Mar 2023
Haller ajumuishwa timu ya Taifa Ivory Coast

Mshambulizi wa kati wa Ivory Coast Sebastien Haller ameitwa kwenye kikosi cha taifa kwa mechi dhidi ya Comoro siku ya Jumatano baada ya kukosekana kwa miezi kadhaa ambapo alipatiwa matibabu ya saratani ya tezi dume

Mshambulizi huyo mwenye umri wa miaka 28 alijiunga na Borussia Dortmund mwezi Julai kutoka Ajax na baadae kugundulika ana saratani

Alifanyiwa upasuaji mara mbili na mizunguko minne ya chemotherapy kabla ya kuanza tena mazoezi mwezi Januari. Alianza kucheza tena Januari 22 na kufunga bao lake la kwanza baada ya kuugua Februari 4 dhidi ya Freiburg

Haller, ambaye amefunga mabao manne akiichezea timu ya taifa ya Ivory Coast, atacheza mechi dhidi ya Comoro Machi 24 na 28 kama sehemu ya kufuzu kwa Kombe la Mataifa ya Afrika 2023.

Winga wa Lille Jonathan Bamba pia ameitwa kwa mara ya kwanza akiwa ameichezea Ufaransa katika ngazi ya vijana.

Ivory Coast ndio wenyeji wa michuano hiyo ambayo imerudishwa nyuma kuanzia Juni na Julai hadi Januari-Februari 2024 ili kuepuka msimu wa mvua

More Stories

Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
8h ago
READ MORE β†’
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
8h ago
READ MORE β†’
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
8h ago
READ MORE β†’
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
12h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
15h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
16h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
16h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
17h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
18h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
19h ago
READ MORE β†’