Mshambulizi wa Tottenham Richarlison na mlinzi wa Paris Saint-Germain Marquinhos wote watakosa mechi ya kirafiki ya Brazil dhidi ya Morocco mnamo Machi 25 kutokana na majeraha, wakiungana na Neymar kwenye orodha ya wachezaji ambao hawapo, kulingana na taarifa iliyotolewa na Brazil
Majeraha hayo mapya yamewaacha mabingwa hao mara tano wa dunia bila ya wachezaji wao nyota huku wakijiandaa kuwavaa Morocco katika mji wa Tangier
Richarlison, 25, aliondoka uwanjani akilia Jumamosi baada ya kuumia mapema katika sare ya 3-3 ya Tottenham dhidi ya Southampton
"Daktari wa timu ya taifa Rodrigo Lasmar aliwasiliana na klabu ya Richarlison, na kubaini kuwa hatakuwa sawa kucheza mechi ya kirafiki," Shirikisho la Soka la Brazil (CBF) lilisema katika taarifa yake Jumamosi jioni.
"Marquinhos, 28, bado anapata nafuu kutokana na jeraha la misuli kwenye tumbo lake na hatakuwa sawa kwa wakati, iliongeza"
Kocha wa muda wa Brazil Ramon Menezes alimwita Yuri Alberto mwenye umri wa miaka 22 wa klabu ya Sao Paulo ya Corinthians kuchukua nafasi ya Richarlison na Bremer mwenye umri wa miaka 26 wa Juventus kuchukua nafasi ya Marquinhos