Tanzania - Taifa Stars - Yanga - Simba

Serikali yaweka Mil 500 Stars kufuzu Afcon 2023

Joel JJ By Joel JJ
β€’
20 Mar 2023
Serikali yaweka Mil 500 Stars kufuzu Afcon 2023

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana amesema Serikali itatoa kiasi cha Shilingi Milioni 500 endapo timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu (Taifa Stars) itafuzu kushiriki Fainali za Kombe la Mataifa Barani Afrika Afcon 2023 michuano itakayofanyika mwakani 2024 nchini Ivory Coast.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Machi 20, 2023 jijini Dar es Salaam, Dkt Chana alisema Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhe. Hamis Mwinjuma ataongoza hamasa kuelekea mchezo dhidi ya Uganda ambao utapigwa March 24 huko Misri na marudiano kupigwa jijini Dar es salaam, March 28.

"Nawaomba Watanzania tujitokeze kwa wingi kuishangilia Taifa Stars katika mchezo wa tarehe 24, Machi 2023 dhidi ya Uganda (The Cranes) ambao utakaochezwa katika mji wa Ismailia nchini Misri na mchezo wa marudiano utachezwa Machi 28, 2023 Uwanja wa Benjamini Mkapa" alisema Mhe. Chana.

Aidha, amewataka wadau wa mchezo huo ikiwemo Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) pamoja na mashabiki kumuunga mkono Kocha wa Timu hiyo Bw. Adel Amrouche, huku akiwasistiza wachezaji wajitume ili waweze kufanya vizuri katika nashindano hayo

More Stories

Mizzima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizzima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
1h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
4h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
5h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
5h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
6h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
7h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
8h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
8h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
21h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
21h ago
READ MORE β†’