Timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' inaendelea kujifua huko Misri kujiandaa na mchezo wa kuwania kufuzu michuano ya Afcon 2023 dhidi ya Uganda
Tanzania inakabiliwa na mechi mbili muhimu dhidi ya Uganda ambazo kama itaweza kushinda zote, itafufua matumaini ya kufuzu kwa Afcon 2023 michuano ambayo itafanyika Januari 2024 nchini Ivory Coast
Tanzania imeweka kambi katika Mji wa Ismailia ambao ndipo mchezo wa kwanza dhidi ya Uganda utapigwa siku ya Ijumaa, saa 11 jioni
Mchezo wa pili utapigwa uwanja wa Benjamin Mkapa, March 28 saa 1 usiku




