Tanzania - Taifa Stars - Yanga - Simba - Azam

Stars matumaini kibao kuelekea mchezo dhidi ya Uganda Cranes

Joel JJ By Joel JJ
β€’
23 Mar 2023
Stars matumaini kibao kuelekea mchezo dhidi ya Uganda Cranes

Kocha Msaidizi wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars), Hemed Morocco, amesema maandalizi yanaendelea vizuri na wanamatumaini makubwa ya kufanya vizuri katika mchezo wa kutasaka nafasi ya kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika (Afcon) 2023 dhidi ya Uganda siku ya Ijumaa

Morocco amesema maandalizi yako vizuri baada ya kufanya mazoezi ya gym ya kutafuta stamina na uwanjani, wachezaji watakuwa fiti kwa ajili ya mchezo huo.

Alisema wachezaji wameanza kuelewana licha ya kukutana muda mfupi, wanaimani nao kupambana katika mchezo huo ili kupata matokeo mazuri .

"Tunatambua mechi itakuwa ya ushindani mkubwa kwa sababu ya ugumu wa mchezo hasa tunapokutana na Uganda, ni imani yangu kwa wachezaji tuliokuwa nao tutapata matokeo mazuri," alisema kocha huyo.

Alisema wanaendelea kufanya mazoezi ya nguvu kuhakikisha wanapata matokeo katika mchezo huo ili kupata kujiweka katika nafasi nzuri ya kufuzu.

Morocco alisema anatumai wanaweza kupata matokeo katika mcheo huo na ule wa marudianoa utakaopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam Jumanne ijayo.

Katika msimamo wa Kundi F, Algeria ipo kileleni ikiwa na pointi sita ikifuatiwa na Niger yenye alama mbili huku Taifa Stars na Uganda zikifuata kutokana na kulingana kila kitu kila moja akiwa na pointi moja.

Timu mbili zitakazoshika nafasi ya juu kutoka katika kila kundi zitafuzu kushiriki michuano hiyo ya Afcon itakayofanyika nchini Ivory Coast baadaye mwaka huu.

More Stories

Mizzima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizzima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
2h ago
READ MORE β†’
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
Klopp amchagua Ter Stegen, kipa namba moja Ujerumani
6h ago
READ MORE β†’
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
6h ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
7h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
8h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
8h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
9h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
9h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
22h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
23h ago
READ MORE β†’