Tanzania - Taifa Stars - Yanga - Simba - Azam

Stars kazi moja dhidi ya Uganda leo

Joel JJ By Joel JJ
28 Mar 2023
Stars kazi moja dhidi ya Uganda leo

Timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' leo inatupa karata muhimu kuwania tiketi ya kufuzu michuano ya Afcon 2023 kwa kuikabili Uganda katika mchezo utakaopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa

Mtananange huo wa dabi ya Afrika Mashariki, utapigwa kuanzia saa 2 usiku

Huu ni mchezo muhimu kwa Tanzania kushinda ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kufuzu michuano ya Afcon 2023 ambayo itafanyika baadae mwaka huu huko Ivory coast

Ushindi kwa Stars dhidi ya Uganda leo utawafanya wafikishe alama saba hivyo kuhitaji alama moja tu katika mechi mbili zitakazokuwa zimebaki dhidi ya Niger na Algeria ili kufuzu

Jana Niger ilichapwa bao 1-0 na Algeria na hivyo kuwahakikisha Algeria kuwa timu ya kwanza kufuzu kwa michuano hiyo baada ya kufikisha alama 12

Tanzania inashika nafasi ya pili ikiwa na alama nne, Niger ni wa tatu wakiwa na alama mbili wakati Uganda wanaburuza mkia wakiwa na alama moja katika kundi F

Stars inahitaji angalau alama nane tu kuweza kufuzu, alama tatu lazima zipatikane kwa Mkapa leo halafu kumaliza kazi hapohapo kwa Mkapa kwenye mchezo utakaofuata dhidi ya Niger mwezi Juni

Habari njema ni kuwa hakuna kiingilio kwa majukwaa ya Mzunguuko, mageti ya dimba la Mkapa yatafunguliwa kuanzia saa sita mchana

Kuwahi kwako uwanjani ndio tiketi yako kwani uwanja utakapokuwa umejaa, mageti yatafungwa!

More Stories

Wamebaki wababe wawili tu wasiofungika Ligi Kuu
Wamebaki wababe wawili tu wasiofungika Ligi Kuu
37m ago
READ MORE →
Afcon haiwezi kuondoka Tanzania, Kenya na Uganda : Motsepe
Afcon haiwezi kuondoka Tanzania, Kenya na Uganda : Motsepe
1h ago
READ MORE →
BREAKING: Tajiri wa Chelsea Boehly ang’atuka kwenye klabu
BREAKING: Tajiri wa Chelsea Boehly ang’atuka kwenye klabu
3h ago
READ MORE →
Ngorongoro Heroes yaweka malengo makubwa CECAFA U20
Ngorongoro Heroes yaweka malengo makubwa CECAFA U20
3h ago
READ MORE →
Yanga SC kukipiga mchezo wa kirafiki na St George uwanja wa Uhuru
Yanga SC kukipiga mchezo wa kirafiki na St George uwanja wa Uhuru
4h ago
READ MORE →
Messi aongeza taji jingine, afikisha mataji 49 katika kazi yake
Messi aongeza taji jingine, afikisha mataji 49 katika kazi yake
4h ago
READ MORE →
Raphinha, Yamal wampa wakati mgumu Mbappe mbio za ufungaji bora La liga
Raphinha, Yamal wampa wakati mgumu Mbappe mbio za ufungaji bora La liga
5h ago
READ MORE →
Manchester United yaanguka Old Trafford, yatupwa nje kwenye Carabao
Manchester United yaanguka Old Trafford, yatupwa nje kwenye Carabao
5h ago
READ MORE →
SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa  Yanga SC “Your next: Yanga”
SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa Yanga SC “Your next: Yanga”
5h ago
READ MORE →
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
7h ago
READ MORE →