Wanawake waliobadili jinsia hawataruhusiwa tena kushindana katika mashindano ya mbio za wanawake bila kujali viwango vyao vya testosterone, rais wa Riadha wa Dunia Sebastian Coe amesema
Coe amesema hakuna mwanariadha aliyebadili jinsia ambaye amepitia balehe ya kiume ataruhusiwa kushiriki katika mashindano ya viwango vya dunia ya wanawake kuanzia Machi 31
Akizungumza baada ya mkutano wa chombo cha maamuzi cha shirikisho la riadha duniani, Coe alisema riadha duniani imeshauriana na wadau yakiwemo mashirikisho 40 ya kitaifa, kamati ya kimataifa ya Olimpiki na makundi ya kimataifa kuhusu suala la wanariadha waliobadili jinsia
"Wengi wa walioshauriwa walisema kuwa wanariadha waliobadili jinsia hawafai kushindana katika michezo ya wanawake," alisema
"Wengi wanaamini kuwa hakuna ushahidi wa kutosha kwamba wanaume waliojibadili kuwa wanawake wana sifa sawa na wanawake wa kibaolojia. Uamuzi tuliochukua naamini ni kwa masilahi bora ya mchezo wetu"