Yanga kuifuata TP Mazembe Alhamisi

Joel JJ By Joel JJ β€’ 29th March 2023


Yanga kuifuata TP Mazembe Alhamisi

Klabu ya Yanga itaondoka nchini kesho Alhamisi kuelekea DR Congo ambako wanakabiliwa na mchezo wa kombe la Shirikisho dhidi ya TP Mazembe

Mchezo huo wa kuhitimisha hatua ya makundi, utapigwa Jumapili, April 02 katika dimba la TP Mazembe, saa 10 jioni

Ni mechi muhimu kwa Yanga kusaka ushindi ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kumaliza kinara wa kundi D

Msafara wa Yanga utajumuisha Mashabiki ambao wanakwenda kuongeza hamasa leo ikiwa siku ya mwisho kujiandikisha zoezi likitarajiwa kufungwa saa 10 jioni

Meneja wa masuala ya Digitali, Priva Abiudi Shayo 'Privaldinho' amesema wakiwa DR Congo wanatarajiwa kuzindua tawi rasmi la klabu hiyo katika Mji wa Lubumbashi

Zaidi ya Wananchi 50 kutoka DR Congo wamejiandikisha kuwa Wanachama wa Yanga ambapo Privaldinho amesema watakabidhiwa kadi zao kwenye hafla ya uzinduzi wa Tawi hilo

Msafara wa Mashabiki wa Yanga unatarajiwa kuondoka jijini Dar es salaam kesho Alhamisi kuelekea DR Congo ambapo watakuwa huko kwa siku tatu, timu itarejea nchini April 03 baada ya mchezo dhidi ya TP Mazembe


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.