Manchester City - Liverpool

Halaand hatihati kuwakabili Liverpool Jumamosi

Joel JJ By Joel JJ
β€’
30 Mar 2023
Halaand hatihati kuwakabili Liverpool Jumamosi

Erling Haaland hakuwepo kwenye mazoezi ya Manchester City siku ya Alhamisi. Mshambulizi huyo wa Norway amekuwa katika kiwango kizuri kwa City msimu huu, akifunga mabao 42 katika mechi 37 pekee tangu atue kutoka Borussia Dortmund

Hata hivyo ushiriki wake wikendi hii uko shakani kutokana na jeraha la kinena alilopata katika ushindi wa mabao 6-0 wa Kombe la FA dhidi ya Burnley.

Haaland hakusafiri kuungana na wachezaji wenzake wa kimataifa na Norway alipokuwa akiuguza jeraha lake kwa matumaini ya kuwa sawa kwa pambano kali na Liverpool JumamosiΒ 

Hata hivyo, kukiwa hakuna dalili zozote za mshambuliaji huyo katika mazoezi ya City, kunaweka uhusika wake katika mashaka makubwa.

Iwapo atakosa, ataungana na Phil Foden nje ya uwanja baada ya kiungo huyo wa kati wa Uingereza pia kuondolewa kwenye pambano hilo.

Ingawa hali halisi ya jeraha lake haijajulikana, baba yake, Alfie Haaland, alitoa taarifa kuhusu hali yake kwenye TV2 ya Norway ambayo inaweza kuwatia wasiwasi mashabiki wa City.Β 

Alfie Halaand alisema Man City inaweza kufanya kamali kumtumia katika mchezo dhidi ya Liverpool lakini ni wazi atahitaji matibabu maalum ili kuweza kushiriki mchezo huo

More Stories

Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
25m ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
1h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
2h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
3h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
3h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
16h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
16h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
17h ago
READ MORE β†’
Clement Mzize arejea rasmi kikosini baada ya miezi sita nje kwa majeraha
Clement Mzize arejea rasmi kikosini baada ya miezi sita nje kwa majeraha
22h ago
READ MORE β†’