Baada ya muongo mmoja wa ubabe, je, utawala wa Bayern Munich kwenye Bundesliga unaweza kufikia kikomo?
Borussia Dortmund inaweza kupiga hatua kubwa kuelekea kutwaa taji kwa ushindi kwenye Der Klassiker Jumamosi jioni
Dortmund wamebakiza mechi tisa pekee kabla ya kutwaa taji la kwanza la ligi tangu 2011/12 lakini mechi dhidi ya Bayern Munich ndiyo yenye maamuzi zaidi
Lakini wanakwenda kukabiliana na Thomas Tuchel anayewafahamu zaidi akiwa kwenye kundi la upinzani akipanga kuanguka kwao
Kocha wa zamani wa Dortmund Tuchel aliteuliwa kuchukua nafasi ya Naglesmann huko Bayern
Aliiongoza Dortmund kushinda Kombe la Ujerumani mwaka 2017 lakini taji la kwanza la Bundesliga sasa liko machoni pake
Kwa kuzingatia kuondoka kwa ghafla kwa Nagelsmann, Tuchel alianza kufanya kazi na kikosi cha Bayern Jumatatu
Ni wazi hakuwa na mawasiliano na wachezaji wengi wa klabu hiyo kutokana na majukumu yao ya timu za Taifa
Hilo linamuacha na muda mchache wa kuweka mawazo yake kwenye timu lakini uwepo wake unaweza kuwaongezea wachezaji morali kuwania ushindi mbele ya Dortmund