Shaw akerwa kipigo Newcastle United

Joel JJ By Joel JJ β€’ 3rd April 2023


Shaw akerwa kipigo Newcastle United

Mlinzi wa kushoto wa Manchester United amesema kichapo cha 2-0 dhidi ya Newcastle United ni matokeo yasiyokubalika

Aidha Shaw amesema walistahili kupoteza mchezo huo wa ligi kuu ya Premia kwa sababu hawakujituma zaidi ya wapinzani wao

Kikosi cha Erik ten Hag kilishuka hadi nafasi ya nne kwenye jedwali baada ya kichapo hicho cha Newcastle katika mbio za kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa msimu ujao.

Takwimu sio nzuri kwao kwani hawajashinda au kufunga katika mechi zao tatu zilizopita za ligi

"Walipambana zaidi na kuonekana wanauhitaji mchezo zaidi kuliko sisi," Shaw aliambia Sky Sports.

"Sidhani Newcastle walishinda kwa ubora, walishinda kwa hamu, shauku, njaa, mtazamo. Tunahitaji kutambua matatizo yetu haraka na kuibadilisha. Bado tunaweza kuwa na msimu mzuri sana lakini kwa matokeo na uchezaji kama huu, hatuwezi"


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.