Lionel Messi hatasaini kandarasi mpya katika klabu ya PSG hadi atakapofahamu mipango yao kwa msimu ujao na ana imani kuwa wanaweza kushindania Champions League
Messi amehitaji kuelewa mkakati wao wa soko la usajili la majira ya kiangazi, iwapo Christophe Galtier ataendelea kuwa meneja msimu ujao au ni nani atakayechukua nafasi yake, pamoja na maelezo mengine ya kiufundi kama vile Luis Campos ataendelea kuwa mkurugenzi wa michezo.
Kimsingi, Messi mwenye umri wa miaka 35 anataka kuwa na uhakika wa kuwa na timu ya ushindani kujaribu kushinda Ligi ya Mabingwa mwakani katika ambayo itakuwa moja ya misimu yake ya mwisho barani Ulaya
Messi ana ofa kutoka klabu mbalimbali akiwa pia anahusishwa na waajiri wake wa zamani Fc Barcelona