Kocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi anatarajiwa kuwasili nchini wakati wowote akitokea Ubelgiji ambako alikwenda kuhuisha hati yake ya kusafiria
Yanga inakabiliwa na mechi mbili za Ligi Kuu kabla ya kuwakabili Rivers United kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza robo fainali kombe la Shirikisho barani Afrika utakaopigwa April 23 huko Nigeria
Keshokutwa Jumanne April 11 Yanga itaikaribisha Kagera Sugar katika mchezo wa ligi kuu utakaopigwa uwanja wa Azam Complex. Jumapili April 16 mchezo wa pili dhidi ya Simba utapigwa uwanja wa Benjamin Mkapa
Nabi alilazimika kusafiri Ubelgiji kuhuisha hati yake ya kusafiria akikosa safari ya Yanga DR Congo kuhitimisha hatua ya makundi ya Shirikisho dhidi ya TP Mazembe
Amekosa mechi mbili, mchezo wa robo fainali kombe la FA dhidi ya Geita Gold ukiwa wa pili Yanga ikitinga nusu fainali kwa ushindi wa bao 1-0



