Yanga - Local

Ligi Kuu NBC, mechi mbili leo April 11

Joel JJ By Joel JJ
11 Apr 2023
Ligi Kuu NBC, mechi mbili leo April 11

Mikiki mikiki ya ligi kuu ya NBC inaendelea leo kwa mechi mbili kupigwa jijini Dar es salaam

Saa 10 jioni KMC itakuwa uwanja wa Uhuru kumenyana na Geita Gold katika mchezo ambao KMC wanahitaji ushindi ili kujiondoa katika janga la kushuka daraja

KMC wako kwenye eneo la Play-off nafasi ya 14 wakiwa na alama 26 lakini hali ni shwari kwa wapinzani wao Geita Gold ambao wanashika nafasi ya sita wakiwa na alama 34

Saa 1 usiku mabingwa watetezi Yanga watakuwa uwanja wa Azam Complex, Chamazi kukabiliana na Kagera Sugar

Yanga inawania ubingwa wa 29 katika historia lakini Kagera Sugar nao wanahitaji ushindi ili kujiweka katika nafasi nzuri kuepuka hatari ya kushuka daraja

Ushindi wa mabao 2-0 ambao Simba waliupata dhidi ya Ihefu Fc hapo jana ni wazi umewaongezea presha Wananchi kuelekea mchezo huo kwani sasa wanaongoza ligi kwa tofauti ya alama tano, mambo yanaweza kuwa magumu kama watakosa ushindi leo

Simba na Yanga zitachuana kwenye mchezo wa dabi Jumapili, April 16, kama Yanga itapoteza leo na pia kufungwa na Simba ni wazi mbio za ubingwa zitakuwa wazi

More Stories

Wamebaki wababe wawili tu wasiofungika Ligi Kuu
Wamebaki wababe wawili tu wasiofungika Ligi Kuu
4h ago
READ MORE →
Afcon haiwezi kuondoka Tanzania, Kenya na Uganda : Motsepe
Afcon haiwezi kuondoka Tanzania, Kenya na Uganda : Motsepe
5h ago
READ MORE →
BREAKING: Tajiri wa Chelsea Boehly ang’atuka kwenye klabu
BREAKING: Tajiri wa Chelsea Boehly ang’atuka kwenye klabu
7h ago
READ MORE →
Ngorongoro Heroes yaweka malengo makubwa CECAFA U20
Ngorongoro Heroes yaweka malengo makubwa CECAFA U20
7h ago
READ MORE →
Yanga SC kukipiga mchezo wa kirafiki na St George uwanja wa Uhuru
Yanga SC kukipiga mchezo wa kirafiki na St George uwanja wa Uhuru
8h ago
READ MORE →
Messi aongeza taji jingine, afikisha mataji 49 katika kazi yake
Messi aongeza taji jingine, afikisha mataji 49 katika kazi yake
8h ago
READ MORE →
Raphinha, Yamal wampa wakati mgumu Mbappe mbio za ufungaji bora La liga
Raphinha, Yamal wampa wakati mgumu Mbappe mbio za ufungaji bora La liga
9h ago
READ MORE →
Manchester United yaanguka Old Trafford, yatupwa nje kwenye Carabao
Manchester United yaanguka Old Trafford, yatupwa nje kwenye Carabao
9h ago
READ MORE →
SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa  Yanga SC “Your next: Yanga”
SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa Yanga SC “Your next: Yanga”
9h ago
READ MORE →
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
11h ago
READ MORE →