Barcelona walipoteza nafasi ya kujiimarisha kileleni mwa La Liga kwa alama 15 baada ya kulazimishwa suluhu ya bila kufungana nyumbani dhidi ya Girona.
Robert Lewandowski alipata nafasi ya dhahabu ya kufunga bao baada ya dakika nne, lakini akapaisha
Kipa wa Girona, Paulo Gazzaniga, kwa mkopo kutoka Fulham, alikuwa shujaa wa mchezo huo akiokoa michomo mingi iliyoelekezwa langoni kwake
Ni mara ya tatu tu msimu huu kwa Barcelona kudondosha pointi nyumbani. Lakini licha ya matokeo hayo, kikosi cha Xavi kiliongeza faida yao dhidi ya Real Madrid hadi pointi 13 baada ya wapinzani wao kufungwa na Villarreal siku ya Jumapili