Wekundu wa Msimbazi Simba Sc leo wametakata uwanja wa Benjamin Mkapa mbele ya watani zao Yanga waliibuka na ushindi wa mabao 2-0 katika mchezo wa ligi kuu ya NBC
Simba iliingia kwenye mchezo huo leo ikiwa na dhamira ya kusaka ushindi, na iliwachukua dakika mbili tu kufunga bao la kuongoza kupitia kwa Hennock Inonga akitumia vyema makosa ya safu ya ulinzi ya Yanga baada ya mpira wa kona
Kibu Denis akaiongezea Simba bao la pili kwenye dakika ya 32 akikiga shuti kali kutoka takribani mita 25 na kumshinda mlinda lango wa Yanga Djigui Diarra
Simba ilikuwa hatari kupitia mashambulizi ya kushitukiza na pengine walistahili kwenda mapumziko wakiwa na uongozi mnono zaidi kutokana na mfululizo wa mashambulizi waliyotengeneza
Kipindi cha pili Yanga ilirejea ikiwa imara zaidi hasa baada ya kuwaingia Stephane Aziz Ki na Mudathir Yahya lakini haikuwa rahisi kwao kuweza kuipenya ngome ya Simba ilikuwa chini ya Hennock Inonga na Joash Onyango huku mlinda lango chipukizi Ali Salim akiwa bora katika mechi yake ya kwanza ya derby
Simba imefufua matumaini katika mbio za ubingwa ikifikisha alama 63 sasa wakiwa nyuma kwa tofauti ya alama tano dhidi ya Yanga iliyobaki na alama 68
