Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Simba Ahmed Ally amesema maandalizi kuelea mechi dhidi ya Wydad Athletic yameanza leo kikosi cha Simba kikiingia kambini kwa ajili ya mchezo huo wa robo fainali ligi ya mabingwa barani Afrika
Mchezo utapigwa Jumamosi, April 22 saa 10 jioni katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Akizungumza katika Mkutano na Wanahabari kuelekea mchezo huo, Ahmed alisema Simba itaanza kujifua Mo Simba Arena leo saa 10 jioni
"Kikosi kimeingia kambini kwa ajili ya maandalizi ya kuikabili Wydad Athletic siku ya Jumamosi, timu imeingia kambini saa 3 asubuhi. Jioni Simba itaendelea na mazoezi Mo Simba Arena"
"Wachezaji Sadio Kanoute aliyekuwa akisumbuliwa na majeraha ya nyonga na Aishi Manula wataripoti kambini kwa ajili ya kufanyiwa tathmini ya majeraha yao na madaktari watatoa mapendekezo yao iwapo waungene na wenzao kambini au bado wanahitaji muda zaidi wa matibabu"
"Augustinr Okrah amepona alirejea mazoezini wiki iliyopita lakini hakuwa fit kuweza kutumika katika michezo iliyopita," alisema Ahmed
Ahmed amesema klabu ya Wydad Athletic itawasili nchini kesho Jumatano pamoja na waamuzi wote wa mchezo huo ambao wanatoka nchi za Senegal na Ivory Coast
Pia kutakuwa na waamuzi wa VAR kwani kuanzia hatua ya robo fainali VAR inatumika
Mechi za robo fainali zitapigwa kwa usaidizi wa VAR waamuzi watawasili Jumatano
Ahmed ametaja viingilio vya mchezo huo; VIP A Tsh 30,000/-, VIP B Tsh 20,000/-, VIP C 10,000/- na Mzunguuko ni Tsh 5,000/-
Pia kuna Mnyama Package maalum kwa ajili ya marafiki wanaonunua tiketi pamoja na Simba Executive ticket inayopatikana kwa Tsh 20,000/-
Platinum pia zipo kwa gharama ya Tsh 150,000/-