Yanga - Local

Job afichua sababu ya kuongeza mkataba Yanga

Joel JJ By Joel JJ
20 Apr 2023
Job afichua sababu ya kuongeza mkataba Yanga

Mlinzi wa kati wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Yanga SC, Dickson Job amesema ilikua lazima aendelee kubaki klabuni hapo, ndio maana akasaini mkataba mpya wa kuendelea kuhudumu kwenye klabu hiyo

Job alikuwa anahusishwa na kujiunga na Vilabu vya Simba na Azam mwishoni mwa msimu huu, huku ikitajwa pia kuwa na dili zingine nje ya nchi, lakini Uongozi wa Young Africans mwishoni mwa juma lililopita ulimsainisha mkataba wa miaka miwili.

Dickson amesema ilikuwa lazima kwake kubaki Young Africans kwani ni timu ambayo amekuwa nayo kwenye wakati mzuri, pia imempa kile ambacho amekihitaji.

"Kikubwa ni kuwashukuru viongozi na mashabiki wote wa Young Africans kwa kuniamini na kuamua kuniongezea mkataba, nami kama mchezaji na nitaendelea kuipambania nembo kila ninapopata nafasi," amesema Job 

Tangu aliposajiliwa Yanga SC, Beki huyo wa kati amekuwa katika kiwango kizuri ndani ya miaka miwili huku akiwa sehemu ya wachezaji wa kikosi cha kwanza na huku akibadilishana nafasi na nyota wengine wa nafasi hiyo kikosini akiwamo nahodha Bakari Mwamnyeto, Yannick Bangala na Ibrahim Abdullah 'Bacca'

Job mwenye bao moja katika Ligi Kuu Bara alikuwa kwenye sehemu ya wachezaji wa timu ya taifa ambayo inacheza michuano ya Kombe la Mataifa kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN) na kwenye michezo ya kuwania kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika 'AFCON 2023'

More Stories

Wamebaki wababe wawili tu wasiofungika Ligi Kuu
Wamebaki wababe wawili tu wasiofungika Ligi Kuu
4h ago
READ MORE →
Afcon haiwezi kuondoka Tanzania, Kenya na Uganda : Motsepe
Afcon haiwezi kuondoka Tanzania, Kenya na Uganda : Motsepe
5h ago
READ MORE →
BREAKING: Tajiri wa Chelsea Boehly ang’atuka kwenye klabu
BREAKING: Tajiri wa Chelsea Boehly ang’atuka kwenye klabu
7h ago
READ MORE →
Ngorongoro Heroes yaweka malengo makubwa CECAFA U20
Ngorongoro Heroes yaweka malengo makubwa CECAFA U20
7h ago
READ MORE →
Yanga SC kukipiga mchezo wa kirafiki na St George uwanja wa Uhuru
Yanga SC kukipiga mchezo wa kirafiki na St George uwanja wa Uhuru
8h ago
READ MORE →
Messi aongeza taji jingine, afikisha mataji 49 katika kazi yake
Messi aongeza taji jingine, afikisha mataji 49 katika kazi yake
8h ago
READ MORE →
Raphinha, Yamal wampa wakati mgumu Mbappe mbio za ufungaji bora La liga
Raphinha, Yamal wampa wakati mgumu Mbappe mbio za ufungaji bora La liga
9h ago
READ MORE →
Manchester United yaanguka Old Trafford, yatupwa nje kwenye Carabao
Manchester United yaanguka Old Trafford, yatupwa nje kwenye Carabao
9h ago
READ MORE →
SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa  Yanga SC “Your next: Yanga”
SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa Yanga SC “Your next: Yanga”
9h ago
READ MORE →
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
11h ago
READ MORE →