Mikiki mikiki ya Ligi Kuu ya NBC inaendelea leo raundi ya 27 ambapo maafande wa Polisi Tanzania watakuwa nyumbani dimba la Ushirika kuumana na Ihefu Fc
Polisi Tanzania iko mkiani kwenye msimamo wa ligi ikikusanya alama 19 baada ya mechi 26
Njia pekee kwa Polisi Tanzania kujinusuru kuteremka daraja ni lazima washinde mechi zote nne zilizosalia huku pia wakiwaombea mabaya wapinzani wao wanaochuana nao chini ya msimamo
Hata hivyo wanakutana na Ihefu Fc ambayo inashika nafasi ya saba ikihitaji ushindi ili izidi kusogea juu kwenye msimamo wa ligi na kujiongezea mapato kutoka kwa Wadhamini
