Msafara wa kikosi cha Yanga umewasili katika Mji wa Uyo nchini Nigeria kuelekea mchezo wa mkondo wa kwanza robo fainali kombe la Shirikisho dhidi ya Rivers United
Mtananga huo ambao utapigwa Jumapili, April 23 utafanyika katika Mji huo
Yanga itakuwa na siku mbili za kufanya maandalizi ya mwisho kuelekea mchezo huo ambao Wananchi wanahitaji ushindi au hata matokeo ya sare ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kutinga nusu fainali kabla kuhitimisha mchezo wa pili nyumbani April 30




