Polisi Tanzania yaichapa Ihefu Fc 2-1

Joel JJ By Joel JJ β€’ 21st April 2023


Polisi Tanzania yaichapa Ihefu Fc 2-1

Polisi Tanzania imeanza mapambano ya kujinusuru kuteremka daraja leo wakipata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Ihefu Fc katika mchezo uliopigwa uwanja wa Ushirika, Moshi

Mabao mawili ya Kelvin Sabato yalitosha kuihakikishia Polisi Tanzania alama tatu ambazo zimewasogeza mpaka nafasi ya 15 wakifikisha alama 22

Ihefu Fc walitangulia kufunga kupitia kwa Adam Adam, hata hivyo vijana wa Mwinyi Zahera walicheza vyema dakika 30 za mwisho na kujihakikishia ushindi huo


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.