Arsenal wana kazi kutwaa ubingwa Uingereza

Joel JJ By Joel JJ β€’ 22nd April 2023


Arsenal wana kazi kutwaa ubingwa Uingereza

Arsenal lazima wafanye ‘kitu cha ajabu’ ikiwa wanataka kuishinda Manchester City na kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Uingereza

Hayo ni maoni kufuatia timu hiyo kutoka sare ya 3-3 dhidi ya Southampton Ijumaa usiku

Kikosi cha Mikel Arteta kilianza vibaya wakiwa nyuma kwa mabao 2-0 baada ya dakika 14 na 3-1 chini baada ya dakika 66 huku vijana wa Arteta wakionekana kuwa kwenye presha kubwa

Hata hivyo mabao ya dakika za lala salama kutoka kwa Martin Odegaard na Bukayo Saka yalipata pointi muhimu na kutoa imani kwamba Arsenal ingali kwenye mbio za ubingwa 

Inayofuata ni mechi kubwa dhidi ya mahasimu wao wa taji Man City Jumatano usiku

Arsenal watahitaji kushinda mchezo huo ili kuwa katika nafasi nzuri ya kuwa mabingwa lakini ni lazima wawaombee mabaya Manchester City wasiweze kushinda mechi zao mbili za viporo

Arsenal imefikisha alama 75 kileleni mwa msimamo wa ligi baada ya mechi 32 wakati Man City wana alama 70 baada ya mechi 30


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.