Simba - Yanga - Local

Ukarabati mkubwa dimba la Mkapa kuanza May

Joel JJ By Joel JJ
24 Apr 2023
Ukarabati mkubwa dimba la Mkapa kuanza May

Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Ally Mayay amesema Uwanja wa Benjamin Mkapa uliopo Dar es salaam utafungwa rasmi Mei, mwaka huu kupisha matengenezo makubwa ya takribani miezi miwili

Licha ya uwanja huo kuelezwa ulishaanza matengenezo madogo madogo huku ukiendelea kutumika kwa mechi kubwa, Mayay amesema kuwa utafungwa baada ya kuanza kwa matengenezo ya eneo la kuchezea.

Amesema matengenezo hayo ya eneo la kuchezea yatasimamiwa na Shirikisho la Soka Barani Afrika 'CAF' kutokana na uwepo wa michuano ya CAF Super Cup

"Sababu kilichokuwa kinafanyika sasa hivi ni matengenezo ya baadhi kama vyumba vya kubadili nguo, maeneo ya wanahabari, vyumba vya waamuzi ambayo ni maboresho madogo lakini yale makubwa yataanza mwezi wa tano ambapo matumizi ya uwanja hayatakuwepo na inatarajia kuwa si chini ya wiki sita mpaka nane," amesema Mayay.

Amesema hayo ni marekebisho ya kawaida kama ilivyoelezwa hapo awali kwani kiwango na ubora wa uwanja hutengenezwa na kutumika kulingana na nyakati husika lakini muda unavyozidi kwenda, inapaswa kufanyiwa maboresho kuendana na nyakati

Kwa maelezo hayo, uwanja huo unaotumika kama uwanja wa nyumbani wa timu za Simba SC na Young Africans, unatarajiwa kutumika na timu hizo kwenye mechi za Robo Fainali za klabu Afrika kabla ya kuanza matengenezo ya eneo la kuchezea.

Na kwa mujibu wa ratiba ya Shirikisho la Soka la Barani Afrika 'CAF' ya mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho la Soka Afrika (CAF) mashindano hayo yanatarajiwa kufikia tamati Juni 11, 2023.

More Stories

Yanga SC kukipiga mchezo wa kirafiki na St George uwanja wa uhuru
Yanga SC kukipiga mchezo wa kirafiki na St George uwanja wa uhuru
55m ago
READ MORE →
Messi aongeza taji jingine, afikisha mataji 49 katika kazi yake
Messi aongeza taji jingine, afikisha mataji 49 katika kazi yake
58m ago
READ MORE →
Raphinha, Yamal wampa wakati mgumu Mbappe mbio za ufungaji bora La liga
Raphinha, Yamal wampa wakati mgumu Mbappe mbio za ufungaji bora La liga
1h ago
READ MORE →
Manchester United yaanguka Old Trafford, yatupwa nje kwenye Carabao
Manchester United yaanguka Old Trafford, yatupwa nje kwenye Carabao
1h ago
READ MORE →
SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa  Yanga SC “Your next: Yanga”
SimbaSC yatuma ujumbe mzito kwa Yanga SC “Your next: Yanga”
1h ago
READ MORE →
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
Barcelona yaendeleza dozi La Liga, yaipiga Racing Santander 7-2
3h ago
READ MORE →
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
Mnyama avunja uteja Chamazi, sasa macho Dabi ya Kariakoo
13h ago
READ MORE →
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
Simba mwendo mdundo, yaichapa Azam Fc 2-0
13h ago
READ MORE →
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
Highlights : Azam Fc 0-2 Simba
14h ago
READ MORE →
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
Mizizima derby pilato Herry Sasii kuwaamua Azam na Simba
17h ago
READ MORE →