Local

Timu ya Msuva kwenye wakati mgumu Saudi Arabia

Joel JJ By Joel JJ
β€’
24 Apr 2023
Timu ya Msuva kwenye wakati mgumu Saudi Arabia

Mshambuliaji wa Kimataifa wa Tanzania, Simon Msuva ambaye anaichezea Al-Qadsiah amesema anaamini kuwa msimu ujao wa soka huko Saudi Arabia unaweza kuwa na neema zaidi kwake kuliko huu unaomalizika

Msuva ambaye huu ni msimu wake wa kwanza kucheza soka la kulipwa nchini humo, amejikuta na chama lake wakiwa kwenye mapambano ya kuhakikisha wanasalia kwenye ligi hiyo badala ya kuwa kwenye vita ya kupanda ligi kuu

Nyota huyo wa zamani wa Wydad Casablanca na Difaa El Jadida za Morocco alisema idadi kubwa ya wachezaji ambao wameingia kwa wakati mmoja kwenye kikosi hicho pengine ni sababu ambayo imechangia

"Tunaweza kubakia kwenye ligi, tupo nafasi moja juu ya hatari ya kushuka daraja, Jumatano tutacheza na maandalizi ya mchezo yapo sawa, ligi ni ngumu sana na kila mmoja wetu hasa ambao ni wageni tumekuwa tukihakikisha tunaizoea na kucheza kwenye viwango vyetu," alisema

"Natamani kwenye uchezaji wangu soka hapa nicheze ligi kuu, najua hilo linawezekana, timu yetu ni nzuri, inaweza kupandambana na kupanda daraja, ni suala la muda, kilichotokea msimu huu haikuwa matarajio yetu lakini tutapambana na kujaribu tena bahati yetu msimu ujao"

Katika Ligi hiyo ya daraja la Kwanza Saudi Arabia, Msuva licha ya ugeni wake ameweka kambani mabao manane na anatarajiwa tena, Jumatano kuongoza mashambulizi ya timu hiyo dhidi ya Al Qaisumah wakiwa ugenini

Al-Qadsiah anayoichezea Msuva ipo nafasi ya 15 wakiwa na pointi 28 kwenye msimamo wa ligi hiyo huku wakipishana mabao tu na Najran ambao wapo kwenye mstari wa kushuka daraja

More Stories

Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
Mo Dewji aichochea Simba, aweka milioni 200 dhidi ya Azam
27m ago
READ MORE β†’
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
BREAKING: Chelsea wagonga hodi PSG kwa Fabian Ruiz
1h ago
READ MORE β†’
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
Pape sakho kutoa nafasi Raja kumsajili Philipinho
1h ago
READ MORE β†’
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
Kocha De Zerbi na Tottenham Yake Mambo magumu, Watolewa kwenye Carabao Cup
2h ago
READ MORE β†’
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
Azam FC dhidi ya Simba leo, hatumwi mtoto dukani
3h ago
READ MORE β†’
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
Patrice Motsepe kuwasili Tanzania kwa ukaguzi wa maandalizi ya AFCON 2027
3h ago
READ MORE β†’
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
Alama tatu za jasho na damu kwa Yanga SC...! Yanga 1-0 Geita Gold
16h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
Highlights : Yanga 1-0 Geita Gold
16h ago
READ MORE β†’
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
Hatimaye Yanga waonja uchungu wa red card baada ya Aziz Ki kuonyeshwa kadi nyekundu
17h ago
READ MORE β†’
Clement Mzize arejea rasmi kikosini baada ya miezi sita nje kwa majeraha
Clement Mzize arejea rasmi kikosini baada ya miezi sita nje kwa majeraha
22h ago
READ MORE β†’